YANGA YAENDELEA KUTETEMA KWA 2 : 0 KWA DODOMA JIJI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 15 May 2022

YANGA YAENDELEA KUTETEMA KWA 2 : 0 KWA DODOMA JIJI



WAKIWA Uwanja wa Jamhuri,Dodoma leo Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 Dodoma Jiji na kufanya waweze kusepa na pointi tatu.

Ni mabao ya Dickosn Ambundo dk ya 11 na bao la pili lilifungwa na kipa wa Dodoma Jiji,Mohamed Yusuph dk ya 35 katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Zawadi Mauya jamo lililomfanya ajifunge.


Kinara wa mabao ndani ya Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa yeye kutokufunga sio tatizo kikubwa ni ushindi wa timu.
“Nimekuwa nikipata nguvu ya kuendelea kupambana licha ya mabeki kuweza kunikamia wakitaka nisiweze kutetema kwenye mechi ambazo wanacheza wanahitaji nisiteteme.


“Ushindi wa timu ni kitu cha msingi kisha mimi ninakuwa na kazi ya kutimiza majukumu yangu hasa kwa malengo ambayo ninakuwa nimejiwekea,” amesema.


Yanga inafikisha pointi 60 ikiwa imecheza mechi 24 ndani ya Ligi Kuu Bara na haijapoteza mchezo mpaka sasa.


Kiungo wa Dodoma Jiji, Hassan Nassoro aliweza kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dk ya 88 kwa kumchezea faulo Yannic Bangala.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso