Mamilioni ya waislamu kwenye mataifa kadhaa duniani leo wanasherehekea sikukuu ya Eid Al-Fitr baada ya kukamilika kwa nguzo muhimu ya kidini ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Sherehe za mwaka huu zinafanyika chini ya kiwingu cha kupanda kwa bei za vyakula ulimwenguni kulikochochewa na vita vinavyoendelea nchini Ukraine huku maeneo mengine yakiwa bado yanaandamwa na mizozo.
Nchini Indonesia, taifa lenye idadi kubwa ya waislamu duniani, sherehe ya Eid inaadhimishwa leo kwa uhuru mkubwa baada ya kuondolewa kwa vizuizi vya kukabiliana na janga la virusi vya corona vilivyodumu kwa miaka miwili.
Sikukuu ya Eid, moja ya sherehe muhimu katika kalenda ya Waislamu huadhimishwa kwa ibada ya pamoja, dhifa ya chakula, manunuzi ya nguo mpya na waumini kutembeleana.
Chanzo:DW
No comments:
Post a Comment