SIMBA WAENDELEA KUANDAMWA NA SARE MECHI NNE MFULULIZO LIGI KUU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 3 May 2022

SIMBA WAENDELEA KUANDAMWA NA SARE MECHI NNE MFULULIZO LIGI KUU

 



KLABU ya Simba Sc imelazimisha sare ya 2-2 dhidi ya timu ya Namungo Fc mchezo wa ligi ambao ulipigwa kwenye dimba la Ilulu Mkoani Lindi ambao ni mchezo wa awamu ya pili msimu huu ukiwa na mchezo wa marudiano.

Namungo ilianza kupata bao kupitia kwa kiungo wao Jacob Masawe ambaye alipachika bao kali baada ya kupigwa kona na Shiza Kichuya na kumalizia nyavuni.

Simba Sc iliandelea kutafuta bao lakusawazisha kwa kujaribu kutengeneza nafasi nyingi lakini baadae walibahatika kusawazisha bao kupitia kwa Shomari Kapombe.

Mechi mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 1-1 kabla ya Obrey Chirwa kupachika bao la kuongoza kwa timu yake na baadae dakika za lala salama Simba Sc kusawazisha kupitia kwa Kibu Dennis.

Mchezaji wa Namungo Fc, Hashimu Manyanya alipewa kadi nyekundu mara baada ya kuoneshwa kadi za njano mbili kwa utovu wa nidhamu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso