MWANAMKE AUAWA AKIWA LODGE-KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 24 May 2022

MWANAMKE AUAWA AKIWA LODGE-KAHAMA







                  
                             Na Marco Mipawa - Kahama


Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Zuena au Ashura Salum (25-30) mkazi wa Dar es Salaam, amekutwa chumbani akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu na mtu anayedhaniwa kuwa ni mwenza wake katika nyumba ya kulala wageni ya Kalunde iliyoko mjini Kahama, usiku wa kuamkia Mei 22, 2022.


Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, Zuena na mwanaume huyo waliingia chumbani hapo majira ya saa 11:00 alfajiri na kwamba mwanaume alitoka na kutokomea kusikojulikana kabla ya wahudumu wa nyumba hiyo kugundua mauaji hayo.


Kyando amesema, mapema asubuhi siku hiyo wahudumu wa nyumba hiyo waliukuta Mwili wa marehemu chumbani pamoja na simu mbili zenye laini zinaonesha majina hayo.


Amesema jeshi la polisi linaendelea kufuatilia tukio hilo, huku akitoa Rai kwa jamii kujihadhari na watu wasiotambulika vizuri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso