MREMBO AVISHWA PETE YA UCHUMBA MSIBANI MBELE YA JENEZA LA BABA YAKE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 18 May 2022

MREMBO AVISHWA PETE YA UCHUMBA MSIBANI MBELE YA JENEZA LA BABA YAKE
Raia mmoja kutoka katika Jimbo la Limpopo nchini Afrika Kusini ameibua mjadala baada ya kuweka video yake katika mtandao wa TikTok ikimuonyesha akimvisha pete ya uchumba mchumba wake mbele ya Jeneza la baba wa msichana huyo.


Mtumiaji huyo wa mtandao wa TikTok anayetumia jina la M.Mojela aliweka video hiyo mwanzoni mwa wiki hii ikimuonyesha akipiga goti moja ishara ya kumuomba mpenzi wake akubali kuvishwa pete huku msichana huyo akilia.


Katika tukio hilo Jeneza la baba wa msichana huyo linaonekana likiwa umbali wa mita moja kutoka alikopiga goti mwanaume huyo.


Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Afrika kusini wameonyesha kuwa na mawazo tofauti kuhusu tukio hilo huku wengine wakikosoa kitendo hicho.


Bado hakuna mwanafamilia aliyejitokeza kufafanua kuhusu tukio hilo la aina yake la mwanaume kumvisha pete mchumba wake katika msiba wa baba yake


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso