MANARA NA CEO SIMBA KIKAANGONI TFF KESHO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 20 May 2022

MANARA NA CEO SIMBA KIKAANGONI TFF KESHO


MSEMAJI WA YANGA HAJI MANARA

Kamati ya maadili ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) imepanga kukutana kesho Mei 21, 2022 kusikiliza mashauri mawili yaliyowasilishwa mbele ya kamati yake na vilabu vya Simba na Yanga.


Yanga ilimwandikia mwenyekiti wa kamati ya Maadili ikimlalamikia mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez kwa madai kuwa kupitia redio moja nchini Africa Kusini alitoa shutuma zisizo za kweli dhidi ya klabu hiyo hivyo kuchafua taswira ya klabu mbele ya umma.


Nao Simba wanamlalamikia ofisa wa Yanga, Haji Manara kwa madai kuwa kupitia mtandao wake wa kijamii alitoa shutuma zisizo za kweli dhidi ya klabu yao, hivyo kukiuka maadili ya TFF toleo la 2013.

CEO WA SIMBA BABRA

Baada ya klabu hizo kuwasilisha malalamiko hayo, mwenyekiti wa kamati ya maadili aliielekeza sekretarieti ya TFF kuhakikisha walalamikiwa wote wanapewa mashtaka dhidi yao pamoja na wito wa kuhudhuria mashauri hayo ambayo yalianza kusikilizwa Mei 14, 2022.


Hata hivyo taarifa hiyo imesema kikao cha kesho ni mwendelezo wa kamati ya maadili kusikiliza mashauri hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso