MAELFU YA WANANCHI WASUSIA KUTUMIA DAWA ZA VVU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 9 May 2022

MAELFU YA WANANCHI WASUSIA KUTUMIA DAWA ZA VVU




Mamlaka nchini Msumbiji zimesema zaidi ya wagonjwa 14,000 wa VVU wameachana na tiba ya kurefusha maisha inayotumika na wagonjwa wa VVU katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka katika jimbo la kati la Zambézia.


Wagonjwa wa kiume ni sehemu kubwa zaidi ya wale ambao hawatumii tena dawa hizo, kulingana na Dk Cheinaze Veríssimo - mkuu wa mkoa wa Mpango wa VVU katika eneo hilo.


Alilaumu unyanyapaa na ubaguzi unaohusishwa na VVU kwa kiwango kikubwa cha wanaokiuka sheria.


Zaidi ya wagonjwa 300,000 wanatumia dawa za VVU ambazo hurefusha maisha katika mkoa wa Zambézia.


“Changamoto tuliyonayo sasa ni kuhusiana na wale wagonjwa wanaoacha kutumia dawa hizo. Ikiwa mtu ataacha matibabu, virusi hupata nguvu zaidi moja kwa moja, mtu anaugua na hata, wakati mwingine, inaweza kusababisha kifo,’’ Dk Veríssimo alisema.


Alisema maafisa wa afya watakuwa wakipeleka dawa nyumbani kwa wagonjwa ambao hawawezi kwenda kwenye vitengo vya afya - iwe kwa sababu ya ugonjwa au kwa kuogopa kunyanyapaliwa.

CHANZO:BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso