COASTAL UNION KUKIPIGA NA YANGA FAINALI ASFC - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 29 May 2022

COASTAL UNION KUKIPIGA NA YANGA FAINALI ASFC



Wagosi wa kaya Coastal Union wamefanikiwa kutinga fainali kombe la shirikisho la Azam ASFC kwa kuichapa Azam Fc mikwaju ya penati katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa leo katika dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


Na Said Muhibu,Lango la habari


Mechi kati ya Coastal Union dhidi ya Azam Fc ilichezwa kwa dakika 120 huku washambuliaji wa timu zote mbili kutotikisa nyavu, jambo lililopelekea timu zote mbili kufika hatua ya mikwaju ya penati. Coastal Union iliibuka kidedea kwa kuifunga Azam Fc 6-5.


Waliopata penalti kwa Azam FC ni Rodgers Kola, Bruce Kangwa, Never Tigere, Agrey Morris na Idriss Mbombo huku Lusajo Mwaikenda na Charles Zulu wakikosa.


Kwa upande wa Coastal waliopata penati ni Muhsin Makame, Amani Kyata, Pascal Kitenge, William Kising, Moubarack Hamza na Abdul Sopu huku Miraji Hassan akikosa.


Klabu ya Young Africans itavaana na Coastal Union katika mchezo wa fainali kombe la shirikisho la Azam ASFC mnamo Julai 2 mwaka huu.

CHANZO: LANGO LA HABARI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso