CHADEMA NA CCM USO KWA USO WIKI IJAYO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 11 May 2022

CHADEMA NA CCM USO KWA USO WIKI IJAYO





Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Mbowe amewataka viongozi wa CHADEMA kuheshimu vyama vya siasa vingine.


Mbowe ametoa kauli hiyo leo Mei 11, 2022 CHADEMA wakati akihutubia kikao cha Baraza Kuu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam lililohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 400 wa chama hicho wanaotoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.


“Tusipoteze muda kujadili wengine, tutumie muda mwingi kujenga CHADEMA, kujenga CHADEMA yenye ndoto za watu. Lazima tuheshimu vyama vingine vya siasa kwa sababu hujui kesho chama kipi kitakuwa chama kikuu cha upinzani. Tusiwe wepesi wa kushambulia wenzetu kwa sababu huwezi jua huenda uwezo wao umeishia hapo",amesema Mbowe.


"Wiki ijayo tutaanza vikao vya CHADEMA na CCM Tumepanga kukutana Delegation ya CHADEMA yenye wajumbe wasiozidi 10 na Delegation ya CCM wiki inayokuja, tutaenda kuzungumza nini kinafanya taifa letu lisiende mbele. Tunataka kutengeneza mahusiano ya msingi. Watu wetu wamekuwa na hofu kwa sababu ya kutoaminiana. Tunataka kujenga taifa",ameongeza Mbowe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso