JINAMIZI LA PENATI LAENDELEA KUWATESA SIMBA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 24 April 2022

JINAMIZI LA PENATI LAENDELEA KUWATESA SIMBA

 Watanzania wawakilishi, Simba kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho safari yao imefika kikomo leo nchini Afrika Kusini baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalty 4-3.

Mchezo ulikuwa mzito hasa kipindi cha kwanza, Simba walipiga mpira mwingi kwa kujilinda huku viungo wakishindwa kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wao.

Idadi ilikuwa ni 1-1 na kuwafanya Simba waweze kwenda kuamua mchezo kwa mikwaju ya penalti hapo ndipo ugumu unaanzia kutokana na historia ya samba msimu huu hasa katika upigaji wa penati jambo ambalo samba msimu huu kwenye upigaji wa penaji umekuwa mgumu kwao.

Simba ilikosa penati mbili kupitia kwa Jonas Mkude na Henock Inonga huku Aishi Manula akiweza kuokoa penalti moja na ile ya mwisho iliyopigwa na kipa wa Orlando ilizima ndoto za samba za kutinga nusu fainali msimu huu na kuyaaga mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso