BREAKING NEWS: LATRA YATANGAZA NAULI MPYA ZA MABASI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 30 April 2022

BREAKING NEWS: LATRA YATANGAZA NAULI MPYA ZA MABASI



Mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu (LATRA) imetangaza bei mpya za nauli za mabasi na daladala nchini.


Akitangaza kiwango hicho kipya cha nauli leo Jumamosi Aprili 30, 2022 Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Gilliard Ngewe amesema kiwango hicho kipya kitaanza kutumika baada ya siku 14.


Ngewe amesema nauli za daladala kuanzia KM 0-10 nauli itakua Tsh. 500 kutoka Tsh. 400 na KM 11-15 nauli itakua Tsh. 550 kutoka Tsh. 450 na bei ya mwisho ya daladala kwa KM 36 hadi 40 itakua Tsh. 1100 kwa daladala tu.
IMG_20220430_133203



Kwa upande wa nauli za mabasi yaendayo mikoani zimepanda kwa daraja la kawaida ni Tsh. 41.29 kwa KM moja kutoka Tsh. 36.89 huku daraja la kati likipanda kwa shilingi 56.88 kutoka Tsh. 53.22.

Nauli kwa wanafunzi imebakia kuwa Tsh. 200 kwa daladala.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso