TETESI ZA USAJILI LEO JAN 19 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 19 January 2022

TETESI ZA USAJILI LEO JAN 19









Paul Pogba hajaichezea Manchester United tangu alipoumia paja mwezi Novemba


Paris St-Germain wanafanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 28, na kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Franck Kessie, 25, kutoka Manchester United na AC Milan mtawalio. Hatua hiyo pia inatarajiwa kumshawishi mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, tkusalia katika klabu hiyo licha ya kuwa ananyatiwa na Real Madrid. (ESPN)


Mkufunzi wa Roma Jose Mourinho, 58,anasema kuwa amejitolea kwa kalbi hiyo na kujitenga na Everton baada ya madai kuibuka kuwa ni mmoja wa makocha wanaopigiwa upato kuchukua nafasi ya Rafael Benitez. (Sky Sports)

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 18.01.2022


Newcastle wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Adana Demirspor na Italia Mario Balotelli, 31, kulingana na rais wa klabu hiyo ya Uturuki Murat Sancak. (Inside Futbol via Star)





Newcastle wanafikiria kumsajili Mario Balotelli


Juventus wamefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Ufaransa na Manchester United Anthony Martial lakini mabingwa hao wa Serie A bado hawajawasiliana na klabu hiyo ya Old Trafford kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo wa miaka wa 26. (Goal)



Juhudi za Arsenal za kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Juventus Arthur Melo, 25, zimeimarika baada ya klabu yake ya Itaila kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Lyon wa miaka 24- Mbrazil Bruno Guimaraeskuchukua nafasi hiyo. (Get French Football via Sun)


Juventus pia wamewasiliana na kiungo wa kati wa Uswizi na Borussia Monchengladbach Denis Zakaria, 25, kuchukua nafasi ya Arthur. (90min)





Kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo alijiunga na Juventus kutoka Barcelona kwa kima cha euro mlioni 82


Arsenal wamepata pigo katika juhudi zao za kumsaka mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic, 21, baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia kudai anataka kujiunga na Juventus pekee. (Mail)

Tottenham bado wanajaribu kumsaini winga wa Uhispania Adama Traore Januari hii licha ya kocha wa Wolves Bruno Lage kumshinikiza kiungo huyo wa miaka 25 kusalia katika klabu hiyo hadi mwisho wa msimu. (Fabrizio Romano)

Spurs pia wanajaribu kuwauza wachezaji kama kiungo wa kati wa Ufaransa wa miaka 25 Tanguy Ndombele, beki wa Jamhuri ya Ireland Matt Doherty, 30, kiungo wa Uingereza Dele Alli, 25, na winga wa Uholanzi wa miaka 24 Steven Bergwijn. (Fabrizio Romano)




Tottenham bado wanajaribu kumsaini winga wa Uhispania Adama Traore

Mshambuliaji wa Croatia fIvan Perisic hataondoka Inter Milan mwezi huu wa Januari licha ya tetesi zinazomhusishana Chelsea. Mkataba wa kungo huyo wa miaka 32-unakamilika mwezi Juni lakini Inter inapanga kurefusha mkataba. (Fabrizio Romano)

Inter Milan pia wanafuatilia hali ya are Paulo Dybala,28, Juventus huku mkataba wa mshambuliaji huyo wa Argentina ukielekea kukamilika msimu huu wa joto. (Gazzetto dello Sport via Mail)


Barcelona na Bayern Munich wanaongoza katika mbio za kumsaka beki wa Chelsea Andreas Christensen,25, huku mlinzi huyo wa Denmark akikataa ofa za klabu za Uingereza kwa heshima ya the Blues. (Fabrizio Romano)




Barcelona na Bayern Munich wanaongoza katika mbio za kumsaka kiungo wai Chelsea Andreas Christensen(kulia)

Barcelona pia wana mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 22, kutoka Real Sociedad wakishindwa kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21. (90min)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso