TETESI ZA USAJILI 29 SEPTEMBER - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 28 September 2021

TETESI ZA USAJILI 29 SEPTEMBER

 

Kelvin Phillips

CHANZO CHA PICHA,JUSTIN TALLIS/GETTY IMAGES

Manchester United imeamua kuelekeza nguvu zake kwa kiungo wa Leeds United Kalvin Phillips, 25, baada ya kuachana na mipango yao ya kumsajili kiungo mwenzake wa England Declan Rice, 22, kutoka West Ham. (Star)

West Ham ina mpango wa kumuuza Rice kwa dau la £90m ikijiandaa na dau la kumpata mrithi wake. (Football Insider)

Real Madrid wanafikiria kupeleka ofa kwa ajili ya mlinzi wa pembeni wa Hispania Pedro Porro, 22, ambaye yuko kwa mkopo Sporting Lisbon akitokea klabu ya Manchester City. (O Jogo - in Portuguese)

Franck Kessie

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Franck Kessie

Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vya Uingereza vinavyotajwa kumfuatilia kiungo wa Ivory Coast Franck Kessie, 24, ambaye amegoma kusaini mkataba mpya na klabu yake ya AC Milan. (90min)

Meneja wa Everton Rafael Benitez anataka kuwasajili kiungo wa Hispania Isco, 29 na mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic, 23, pale Goodison Park wakitokea Real Madrid kwa mkataba mfupi wa mkopo mwezi Januari. (Defensa Central - in Spanish) 

Crystal Palace wanamfuatilia kwa makini Tom Davies, 23 wa Everton kufuatia hali ya sintofahamu ya mustakabali wa kiungo huyo wa kingereza. (Football Insider)

Barcelona bado ina nia ya kutaka kumsajili mlinzi wa Juventus na timu ya taifa ya Uholanzi Matthijs de Ligt, 22, na iko tayari kumtoa golikipa mjerumani Marc-Andre ter Stegen, 29, na mshambuliaji mholanzi Memphis Depay, 27, kama sehemu ya kukamilisha mpango huo. (Calciomercato - in Italian)

Isco

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Barca pia inataka kumsajili kiungo kinda raia wa Sweden mwenye umri wa miaka 17 Williot Swedberg kutoka Hammarby. (Expressen - in Swedish)

Mshambuliaji wa Club Brugge Noa Lang yuko tayari kutua Arsenal lakini washika bunduki hao wa London wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan wanaomtaka pia mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 22. (Voetbal24 via Mirror) 

Mtendaji mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke anasema Real Madrid ni klabu "inayomshawishi" Erling Haaland, 21, wakati huu mshambuliaji huyo wa Norway akiangalia mustakabali wake wa baadae. (AS - in Spanish)

Vilabu vya Dortmund na Hoffenheim vinamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Uingereza kutoka West Bromwich Albion mwenye umri wa miaka 17 Reyes Cleary. (Mail)

Jacob Ramsey, kiungo kinda wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 19, anaripotiwa kutakiwa na Manchester City, huku mabingwa hao wa ligi kuu England wakimfuatilia kwa karibu Muingereza huyo. (Fichajes - in Spanish)

Erling Braut Halaand

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kiungo wa zamani wa Hispania Juan Mata, 33, anaangalia mustakabali wake kufuatia kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara Manchester United msimu huu. (Manchester Evening News)

Kiungo wa Roma Steven Nzonzi anakaribia kutua klabu ya Al Rayyan ya Qatari ambapo dirisha la usajili huko linafungwa Septemba 30 na mkataba wa kiungo huyo mfaransa mwenye umri wa miaka 32 unamalizika mwaka 2022. (Calciomercato - in Italian

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso