TETESI ZA USAJILI AUGUST 18 ,2021 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 18 August 2021

TETESI ZA USAJILI AUGUST 18 ,2021






CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,

Christiano Ronaldo


Wakala wa mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo', Jorge Mendes ameipatia Manchester City ofa ya kumsajili nyota huyo wa Portugal mwenye umri wa miaka 36. (Corriere dello Sport - in Italian) (Corriere dello Sport - in Italian)


Lakini City inasisitiza kwamba bado inamlenga mshambuliaji huyo wa Tottenham na England Harry Kane, 28,. (Mirror)


Baada ya kukosa mazoezi na ushindi dhidi ya City, Kane ataichezea Spurs katika Ligi ya Europa dhidi ya klabu ya Porugal Paços de Ferreira Alhamisi. (Guardian)


Arsenal imeanzisha tena mazungumzo na Sheffield United juu ya makubaliano ya mlinda lango, 23, wa England Aaron Ramsdale, baada ya Blades kusemekana kwamba wamepunguza dau lao kutoka £35m hadi £24m. (The Athletic, subscription required)



CHANZO CHA PICHA,PA MEDIA
Maelezo ya picha,

Aaron Ramsdale

Na kocha wa Sheffield United Slavisa Jokanovic amekubali kuwa Ramsdale anataka kujiunga na Arsenal. (Mirror)

Paris St-Germain haijaondoa uwezekano wa uhamisho wa dakika za mwisho wa viungo wa kati raia wa Ufaransa Paul Pogba, 28, kutoka Manchester United na Eduardo Camavinga,10 kutoka Rennes. (L'Equipe - in French)


PSG ina nia ya kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kwa Real Madrid msimu huu. (Mundo Deportivo - in Spanish)


Tottenham inafikiria uhamisho wa mlinzi wa Chelsea Kurt Zouma. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 26, pia amehusishwa na uhamisho wa West Ham msimu huu. (Sky Sports)



CHANZO CHA PICHA,EPA


Atletico Madrid imeiambia Arsenal na Manchester United kwamba beki wa kulia wa England Kieran Trippier, 30, hauzwi. (AS)


Uhamisho wa kudumu wa Martin Odegaard kutoka Real Madrid hadi Arsenal unakaribia huku kukiwa na taarifa kwamba kiungo huyo wa kati, 22 hakushiriki mazoezi na timu ya Real Jumanne. (The Athletic, subscription required)

Wolverhampton Wanderers inajitayarisha kutoa ofa ya £21m kwa Valencia ikimlenga winga wa Ureno Goncalo Guedes, 24. (Birmingham Mail)


Kocha wa Newcastle Steve Bruce anamuwinda kiungo wa kati wa Leicester Hamza Choudhury, 23, kwa mkopo. (Mail)



CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES


Mchezaji wa Everton James Rodriguez amekanusha taarifa kwamba anatafuta uhamisho wa kjuelekea Atletico Madrid, baada ya ujumbe wa Twitter wa mchezaji huyo, 30, wa Colombia kuchukuliwa kama kidokezo kwamba anahamia kwa mabingwa wa La Liga. (Liverpool Echo)

Watford inakaribia kukubali kima cha £7.5m kwa ajili ya mlinzi Mbrazil wa klabu ya Torino Lyanco, 24. (Sky Sports)


Kiungo wa kati wa Manchester United Andreas Pereira, 25, huenda anakaribia kuondoka Old Trafford huku kukiwa na tetesi kwamba anaelekea Flamengo kufuatia mapendekezo mengi ya mkopo kwa Mbrazil huyo. (Mirror)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso