TETESI ZA SOKA ULAYA TAREHE 26 MAY 2021 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 26 May 2021

TETESI ZA SOKA ULAYA TAREHE 26 MAY 2021

Wolves wamejiandaa kumuuza kiungo wao Ruben Neves kwa pauni milioni 35 ili kupata pesa ya kukijenga kikosi chao kwa ajili ya kocha yeyote atakayechukua nafasi hiyo kufuatia kuondoka kwa Nuno Espirito Santo. (The Athletic - subscription required)



Ruben Neves wa Wolves (kulia) alishawahi kuzivutia klabu vigogo za England Man City na Man United

Wolves hata hivyo hawatalazimika kumuuza Neves, 24, ambaye amekuwa katika klabu hiyo tangu mwaka 2017, lakini watasikiliza ofa yoyote kama itaiwezesha kukijenga upya kikosi chao. (Express & Star)

Mchezaji nyota wa Brazil Philippe Coutinho, 28, atakuwa miongoni mwa wachezaji 10 walioorodheshwa kuuzwa na Barcelona katika dirisha la usajili la mwisho wa msimu huu. (Star)


Philippe Coutinho ni miongoni mwa wachezaji 10 wanaotarajiwa kuuzwa na Barcelona


Barcelona na Manchester City ni miongoni mwa klabu zinazomtaka kiungio wa kati wa klabu ya Atalanta Mjerumani Robin Gosens, 26. (Sport)


Man United wamekubali kusaini mkataba na mlinda mlango wa Aston Villa Muingereza Tom Heaton, 35, kwa uhamisho huru mwezi ujao. (Express)


Wilfried Zaha


Tottenham na Everton wanataka kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 28, kwa pauni milioni 40. (Goal)


West Ham wanamtaka kiungo wa klabu ya Spartak Moscow na Jamuhuri ya Czech, Alex Kral, 23. (Sky Sports)


Willian atamani kurudi Chelsea ikiwa ni miezi 10 tu toka ajiunge na Arsenal


Mshambuliaji wa Arsenal Mbrazili Willian, 32, anataka kurejea katika kikosi cha Chelsea - ikiwa ni chini ya miezi 12 baada ya kuihama klabu hiyo aliyokaa nayo kwa miaka saba. (Sky Sports)


Mlinzi wa Villarreal Pau Torres, 24, amekataa kujadili kuhusu tetesi zijazomuhusisha na kuhamia Manchester United msimu huu, kabla ya mchezo wa Jumatano wa fainali za Europa dhidi ya United. (Metro)


Hudson-Odoi

Chelsea huenda wanataka kumuuza kiungo wao wa kati Muingereza Callum Hudson-Odoi,mwenye umri wa miaka 20, huku akitarajiwa kwenda Borussia Dortmund . Dortmund pia wanaweza kuangalia uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa safu ya mbele wa Leeds United Mbrazili Raphinha, 24. (Eurosport)

CHANZO CHA HABARI 
BBC - SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso