KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI WA NAFASI ZA MASOMO KWA NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2021/2022. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 20 May 2021

KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI WA NAFASI ZA MASOMO KWA NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2021/2022.


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika Vyuo ambavyo si Vyuo Vikuu ama Vyuo Vikuu Vishiriki nchini. Jukumu mojawapo la Baraza ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vya Ufundi nchini yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi. 


Pia Baraza linao wajibu wa kuratibu udahili wa Wanafunzi kwenye Vyuo na kozi/programu zinazotambulika na mamlaka husika. Baraza (NACTE), linapenda kuufahamisha umma kuwa udahili wa wanafunzi kwa mkupuo wa Septemba 2021 katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote zinazotolewa na Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi utafunguliwa rasmi kuanzia tarehe 27 Mei, 2021 . 

Hivyo, Baraza linawashauri waombaji na wazazi kuzingatia maelezo yatakayotolewa kwenye tarehe tajwa hapo juu. 


IMETOLEWA NA: OFISI YA KATIBU MTENDAJI BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) TAREHE: 17/05/2021


Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yao kuona hilo Tangazo

https://www.nacte.go.tz/wp-content/uploads/2021/05/TANGAZO-LA-UDAHILI-19.05.2021.pdf 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso