JOHN CENA AIOMBA RADHI NCHI YA CHINA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 26 May 2021

JOHN CENA AIOMBA RADHI NCHI YA CHINA






Star wa Mchezo wa mieleka John Cena amechukua hatua ya kuiomba msamaha China kwa kupataja “Taiwan” kama Nchi kauli ambayo ilitafsiriwa kwenda kinyume au tofauti na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika za sheria nchini China.

Kitendo hicho kimefuata baada ya Staa huyo kuinadi filamu aliyoshiriki ya Fast & Furious inayotarajiwa kuingia sokoni siku za hivi karibuni

Hivyo John Cena ali-tuma ujumbe wa msamaha kwa njia ya video kwenye mitandao ya kijamii kwa kuliomba radhi taifa la china kwa kile kilichotafsiriwa kuwa ni tofauti na kanuni kwa kuiita “Taiwan” ni nchi

“I love and respect Chinese. I am very sorry for my mistake. I am so sorry, I apologise” John Cena

Taiwan ni kisiwa kinachojitegemea, huku Mji mkuu ni Taipei ikiwa na idadi ya watu zaidi ya Milioni 23 chini ya kiongozi “Tsai Ingwen”.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso