NAFASI YA MASOMO YA KOZI YA MAENDELEO YA JAMII - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 9 March 2021

NAFASI YA MASOMO YA KOZI YA MAENDELEO YA JAMII

 KARIBU TUKUHUDUMIE


Mkuu wa chuo cha HUHESO INSTITUTE OF JOURNALISM AND  COMMUNITY DEVELOPMENT kilichopo Mjini Kahama ,Anawatangazia wazazi na walezi wote nafasi za masomo Mhula wa kwanza yatakayoanza mwezi April mwaka huu 2021 katika kozi zifuatazo

·       Kozi ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa jamii Ngazi ya Cheti hadi Stashahada (Diploma) (BASIC CERTIFICATE IN COMMUNITY DEVELOPMENT

·       ORDINARY CERTFICATE IN COMMUNITY DEVELOPMENT.

·       DIPLOMA IN COMMUNITY DEVELOPMENT

·       Mafunzo ya komputa (BASIC CERTIFATE IN COMPUTER APPLICATION) kwa Miezi sita na mwaka Mmoja

 

SIFA ZA MWOMBAJI

·       Kwa kozi za Maendeleo ya Jamii  awe amehitimu kidato cha nne na kupata D nne katika masomo yake ya kidato cha nne.

·       Kwa waombaji wa Basic Certificate kwa mwaka mmoja sifa ni lazima awe na D nne za matokeo ya kidato cha nne,

·       Kwa waombaji wa kozi ya Technician Certificate Mwaka Mmoja sifa ni lazima  awe na Cheti cha Level Four au Principal Pass za Kidato cha sita yaani S na E kwenye matokeo ya kidato cha sita.

Pia chuo kina walimu wa kutosha na waliobobea katika fani ya ufundishaji kwa nadhalia na vitendo na chuo kina pokea wanafunzi wote wa kutwa na Hostel zipo.

Fomu za kujiunga na chuo zinapatika chuoni na Huheso Fm Redio  au wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo 0753 444 840 au 0787 360 512

Pia chuo kimesajiliwana NACTE kwa namba REG/BTP/131P

 

Wote Mnakaribishwa


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso