BONANZA LA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA LAKUTANISHA SHULETATU NYAMBULA KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 10 February 2021

BONANZA LA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA LAKUTANISHA SHULETATU NYAMBULA KAHAMA

 Katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi TAASISI YA HUHESO FOUNDATION kwa ufadhili wa FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY kupitia mradi wa MWANAMKE AMKA imefanya Bonanza la siku moja ambalo limefanyika katika shule ya msingi NYAMBULA na kuwakutanisha wanafunzi wa shule tatu huku lengo kuu likiwa ni kutoa elimu kwa wanafunzi juu ya kujiepusha na ukatili wa kijinsia na sehemu sahihi za kuripoyi vitendo hivyo pindi wanapo fanyiwa.



Picha ya Juu: Msimamizi wa Mradi Joyce Michael kutoka HUHESO Foundation akiongea na Wanafunzi Kuhusu Ukatili wa Kijinsia kwenye Bonanza

Picha ya juu: Gelad Muheto kutoka HUHESO Foundation akiongea na Wanafunzi Kuhusu Ukatili wa Kijinsia kwenye Bonanza



Watoto walipata nafasi ya kucheza Netball katika Bonanza lililoandaliwa na Huheso Foundation ya Kahama.

Katika Bonanza hilo ambalo ambalo limefanyika februari, 5/2021 limezikutanisha shule za msingi NYAMBULA, NGURU na BUSOKA licha ya wanafunzi kupewa elimu ya ukatili wa kijinsia huku wakichangamsha akili zao kwa kuulizwa maswali na mratibu mradi wa MWANAMKE AMKA JOYCE MICHAEL na kupewa zawadi lakini pia walipata wasaa wa kushiriki michezo ya mashindano ya mbio, kuvuta kamba, kukimbia na magunia na kucheza mpira wa miguu wavulana na mpira wa mikono kwa wasichana ambapo zawadi zilitolewa kwa washiriki wa michezo hiyo.

PICHA; Wanafunzi walipata nafasi ya kushindana kuvuta kamba ambayo pia kilikuwa kivutio kikubwa kwenye Bonanza hilo

Miongoni mwa zawadi walizopewa wanafunzi katika bonanza hilo ni pamoja na madaftari, kompasi seti, kalamu, rula, penseli, taulo za kike kwa wasichana na mipira minne kwa shule zote tatu.

Wakizungumza katika BONANZA hilo wanafunzi walioshiriki wameonesha kufurahishwa na elimu waliyoipata ya kupinga ukatili wa kijinsia sambamba na zawadi walizopatiwa.

kwa upande wao walimu wa shule za msingi NYAMBULA  na NGURU mwalimu KADOME JUMANNE na mwalimu ESTERIDA GERALD wamepongeza juhudi hizo za kupinga ukatili wa kijisnia kwa wanafunza hali ambayo wamesema itawasaidia wanafunzi hao kujilinda wao wenyewe na kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia pindi vinapotokea.

PICHA: Afisa maendeleo wa Kata ya Ngogwa akiongea na Wanafunzi katika Bonanza lililoandaliwa na HUHESO Foundation

Awali Afisa ustawi wa jamii manispaa ya Kahama ALINDA BWAKOA na Afisamaendeleo kata yangogwa – ESTHER SANGA wamewaasa wanafunzi hao kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi yao huku mratibu mradi wa MWANAMKE AMKA JOYCE MICHAEL akiwahimiza kujiunga kwenye klabu za kupinga ukatili wa kijinsia zilizopo shuleni.

PICHA: Michezo mbalimbali ikiwemo kukimbia ndani ya gunia ilikuwa kivutio kwa washiriki wa bonanza lililoandaliawa na HUHESO Foundation ya Kahama.

Aidha mradi wa MWANAMKE AMKA unatekelezwa katika kata tano za wilaya ya kahama ambazo ni KINAGA, ZONGOMELA, MONDO, NGOGWA na KILAGO kwa ufadhili wa FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY kwa kushirikiana na HUHESO FOUNDATION hatua ambayo inalenga kuielimisha jamii kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso