WACHIMBAJI WADOGO MBOGWE WASHAURIWA KUFUATA KANUNI ZA MSAADA WA KIUFUNDI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 14 March 2026

WACHIMBAJI WADOGO MBOGWE WASHAURIWA KUFUATA KANUNI ZA MSAADA WA KIUFUNDI



*Mbogwe , Geita*


Wachimbaji wadogo wa madini Mkoa wa kimadini Mbogwe wametakiwa kuzingatia Kanuni za Msaada wa Kiufundi zilizotangazwa na Serikali ili kuongeza tija katika uzalishaji na kuepuka migogoro isiyo ya lazima na wawekezaji.


Rai hiyo ilitolewa Machi 13, 2026 na Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa wakati wa ziara yake ya kikazi katika mgodi wa Peter Kisura Kawe na Washirika uliopo wilayani Mbogwe.


Dkt. Kiruswa alisema kuwa ni vyema kuzingatia Kanuni mpya za mwaka 2025 zinazoratibu ushiriki wa watoa msaada wa kiufundi katika leseni ndogo za uchimbaji.


Dkt.Kiruswa alieleza kuwa , mikataba yote ya msaada wa kiufundi kati ya mchimbaji mdogo na mtoa huduma lazima isajiliwe rasmi Tume ya Madini.


Dkt.Kiruswa alifafanua kuwa kanuni zinaelekeza kuwepo kwa uwazi katika mgawanyo wa mapato ya madini yatakayozalishwa ili kumlinda mchimbaji mdogo.


Aliongeza kuwa , msaada wa kiufundi unapaswa kulenga kuongeza ujuzi, kutoa teknolojia ya kisasa, na kuongeza kiasi cha madini kinachopatikana.


Dkt.Kiruswa alisisitiza kuwa,wachimbaji wadogo

wana fursa ya kupata mikopo yenye riba nafuu kupitia programu maalum za kibenki kama CRDB Bank zilizozinduliwa hivi karibuni.


Kwa upande wake Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa kimadini Mbogwe Mhandisi Ludovick Mwacha alisema mpaka sasa mkoa wa kimadini Mbogwe umefikia asilimia 75.81 makusanyo ya lengo la Mwaka 2025/2026.


Awali, akitoa taarifa ya mwenendo wa uzalishaji katika mgodi wa Peter kisura na Washirika , Meneja Mgodi Mhandisi Samson Mathias alisema, mgodi ulianza uzalishaji rasmi mwaka 2025 na mpaka sasa unazalisha kilogram 8 kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso