WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA LEO DESEMBA 05, 2025 AMEKAGUA OFISI YA MTENDAJI WA KATA YA KISESA ILIYOPO HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU MKOANI MWANZA AMBAYO ILIHARIBIWA NA VURUGU ZILIZOTOKEA OKTOBA 29, 2025. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 5 December 2025

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA LEO DESEMBA 05, 2025 AMEKAGUA OFISI YA MTENDAJI WA KATA YA KISESA ILIYOPO HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU MKOANI MWANZA AMBAYO ILIHARIBIWA NA VURUGU ZILIZOTOKEA OKTOBA 29, 2025.


*_Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 05, 2025 amekagua Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kisesa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza ambayo iliharibiwa na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025._*


*DONDOO ZA ALIYOYAZUNGUMZA*


▪️Kila mtumishi wa umma ajikite katika kutatua changamoto za watanzania


▪️Kila mtanzania anaowajibu wa kuipenda Tanzania, tusiyumbishwe na watu wasiotutakia mema, Tanzania ni ya Watanzania tuijenge na tuilinde nchi yetu.


▪️Akitokea mtu anakwambia uharibu mali ya umma, huyo anania ya kuihujumu Tanzania, wakatalieni. Wao, watoto zao na ndugu zao hawaishi hapa Tanzania ila wanafanyia biashara maisha ya Watanzania.


▪️Rais Dkt. Samia alishatoa msamaha kwa vijana walioshiriki kwenye tukio lile bila kutambua wanachofanya, hatutarajii watarudia.


▪️Tanzania ni mwalimu wa masuala ya amani na usuluhisi.


▪️Tusiruhusu uhalifu utawale kwenye nchi yetu, tupo kwenye vita ya kiuchumi, wanamezea mate rasilimali zetu, Tanzania tumegundua madini adhimu na tutakuwa nchi 1 Afrika na ya 9 duniani kuwa na madini haya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso