DPP AMFUTIA KESI YA UHAINI MFANYABIASHARA NIFFER NA MIKA CHAVALA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 3 December 2025

DPP AMFUTIA KESI YA UHAINI MFANYABIASHARA NIFFER NA MIKA CHAVALA


Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amemfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara Jeniffer Jovin (26) maarufu Niffer pamoja na Mika Chavala, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhaini.


Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 3, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Aaron Lyamuya, baada wakili wa Serikali, Titus Aron kuileleza mahakama hiyo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao wawili.




Mapema hii leo Niffer pamoja na Mika Chavala walifikishwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo lililokuwa linawakabili.


Novemba 25, 2025, washtakiwa 20 kati ya 22 waliokuwa wanashtakiwa pamoja na Niffer waliachiwa baada ya DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka yao, hivyo Niffer na Chavala wakaendelea kubaki mahabusu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso