Ujumbe mzito umetolewa kwa kundi la vijana, ambao walitajwa kuingia kwenye mkumbo wa kuiga matukio mabaya bila kutambua athari zake. Vijana wanahimizwa kuona umuhimu wa kuketi na kutumia majukwaa yao ya kidijitali na kijamii kujadili umuhimu wa kulinda amani, maadili, na Utanzania wao.
Habib Sadick, dereva wa bajaji, anatoa Funzo muhimu kwa vijana: "Kama kijana nilikuwa na wajibu wa msingi wa kupiga kura na kuendelea na biashara... Lakini kilichotokea sijawahi kukiona. Sehemu kubwa ya vijana waliofanya hivi vitu... Ni funzo kwa vijana kwamba vijana tusifanye kitu chenye hasara kubwa katika maisha, usikifanye."
2
Salma Juma Kimaro anasisitiza: "Sisi kama Watanzania, vijana wengi wameingia katika mkumbo wa kuiga vitu ambavyo hawavijui." alisema na kusisitiza kuwa vijana wanapaswa kutambua kuwa nguvu yao inapaswa kuelekezwa katika ubunifu na uzalishaji, sio uharib
Mwanasaikolojia wa Jamii Hussein maarifa akizungumza kutoka Lindi anasema: "Kutokana na shinikizo la kijamii au kisiasa, vijana wengi hujiingiza katika makundi ya vurugu. Tunahitaji kuimarisha elimu ya uraia shuleni na vyuoni, kuwafanya vijana wajue wajibu wao kikatiba na kuona thamani ya kuwa watulivu na wabunifu."
Aidha aliwataka vijana kugeuza mitandao yao kuwa daraja la majadiliano chanya kuhusu ulinzi wa amani na usalama wa nchi kuliko kusikiliza na kuiga na kufanya vurugu ambazo athari yake ni kubwa.


No comments:
Post a Comment