Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, Serikali itaendelea kulinda uhuru wa Vyombo vya Habari ili watanzania wapate haki ya kupata habari za ndani na nje ya Nchi.
Rais Dkt. Samia amesema hayo Jijini Dodoma wakati akihutubia Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo, pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa, Serikali itaendelea kutoa leseni kwa vyombo vya habari na kulinda uhuru wa kufanya kazi zao kwa kufuata sheria za Nchi.
Vile vile, amesisitiza kuwa, Serikali itaimarisha Vitengo vya Habari vya Serikali ili viweze kutoa habari kwa weledi na kwa wakati, huku pia akiweka mkazo wa kuwatambua waandishi wa habari za maendeleo nchini kwa kutoa Tuzo za Samia Kalamu Awards.

No comments:
Post a Comment