MWENYEKITI WA SMAUJATA MKOA WA MOROGORO ASHIRIKI MAHAFALI YA KIDINI FDC ILONGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 7 November 2025

MWENYEKITI WA SMAUJATA MKOA WA MOROGORO ASHIRIKI MAHAFALI YA KIDINI FDC ILONGA


Morogoro, Tanzania


Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Morogoro, Shujaa Joyce Hamis Nyangi, ameshiriki mahafali ya kidini yaliyofanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ilonga (FDC), yakihusisha jumuiya za CASFETA na UKWATA.


Shujaa Joyce aliambatana na mashujaa wenzake watatu — Peace Kajei, Mama Seyeye, na Shujaa Shoni, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Makada Walimu Mkoa wa Morogoro.


Katika mahafali hayo, wageni hao wamewahimiza wanafunzi kujiepusha na vitendo viovu na kuzingatia maadili mema.


Akiwa mgeni rasmi, Shujaa Joyce Hamis Nyangi ametoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia, akieleza maana ya ukatili, aina zake, jinsi ya kutoa taarifa (kureport), na mbinu za kujilinda dhidi ya vitendo hivyo.


Aidha, amewahimiza vijana kuilinda amani iliyopo nchini na kutoa taarifa kwa vyombo husika pindi wanapoona viashiria vya uvunjifu wa amani.


Katika hatua nyingine, Shujaa Joyce amewashukuru viongozi wa chuo na watumishi wote kwa ukarimu wao, na akachangia mahitaji ya wanafunzi wa kidini kwa kujitolea pamoja na wageni wengine waalikwa.


Kwa namna ya kipekee, amewapongeza viongozi wa CASFETA na UKWATA kwa ushirikiano na juhudi zao katika kuimarisha malezi bora kwa vijana.


“KATAA UKATILI, WEWE NI SHUJAA!”


















No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso