MARIDHIANO NDIO DIRA: TAASISI ZA KIISLAMU ZATOA TAMKO NYETI, ZAONYA KUSIWE NA ZAWADI KWA WALIOLETA FUJO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 14 November 2025

MARIDHIANO NDIO DIRA: TAASISI ZA KIISLAMU ZATOA TAMKO NYETI, ZAONYA KUSIWE NA ZAWADI KWA WALIOLETA FUJO


Taasisi za Kiislamu Tanzania zimetoa tamko kali la msimamo kuhusu vurugu zilizosababisha hasara kubwa ya watu na mali nchini, huku zikimuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine waliochaguliwa.

Tamko hilo lililosomwa na Shehe Issa Othman Issa, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa BAKWATA, limetoa wito wa maridhiano huku likionya dhidi ya kuwatunuku waliosababisha machafuko.

Alisema tangu awali viongozi wa Taasisi za Kiislamu walifanya juhudi kubwa kuhimiza amani kabla ya uchaguzi na wamesema kazi hiyo wataendelea nayo kwa maslahi mapana ya taifa. Walionya, "Kamwe wasionekane wajinga kwa kuendelea kuhimiza amani ambayo ni kwa faida ya Watanzania wote."

Wawataka waislamu kote nchini na watanzania wote wanaoitakia mema nchi yao kuendelea kudumisha amani na kama kundi lolote likiona kuna haja ya kudai, kuomba au matakwa yoyote ni wajibu wa wanaodai kuzingatia kuwa ni vyema mazungumzo yaendelee na kamwe kwenye vurugu kinachopatikana ni hasara tu

Maridhiano na Pongezi

Tamko hilo lilitamatika kwa mambo muhimu matatu, ikiwa ni pamoja na maombi mahususi kwa Serikali na pongezi kwa uongozi wa nchi:

Maridhiano ya Kisiasa:

Taasisi za Kiislamu zimeiomba Serikali kutafuta fursa ya suluhu na maridhiano, lakini zimetoa onyo kali kwamba maridhiano hayo hayapaswi kuwa zawadi kwa walioleta fujo.

Pongezi:

Wamempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine waliochaguliwa kwa kumaliza salama mchakato wa uchaguzi.

Uchaguzi wa Amani:

Viongozi wa dini na wanasiasa wametakiwa kumuogopa Mwenyezi Mungu na kuacha kuwahamasisha vijana kufanya vurugu. Badala yake, wamehimiza kuwa haki yoyote inayotafutwa, idaiwe kwa njia ya amani na mazungumzo, kwani vurugu haziwezi kuleta haki bali zitaleta maafa.

Msimamo Mzito Kuhusu Vurugu na Uwajibikaji

Akisoma tamko hilo, Shehe Othman alisisitiza kuwa jukumu la kuhimiza amani wataliongoza daima, akionya kusiwepo na kundi linalojiona lina haki zaidi ya kusikilizwa kuliko wengine.

Uchaguzi wa Amani:

Viongozi hao wameendelea kuhimiza Waislamu kote nchini na Watanzania wote wanaoitakia mema nchi yao kuendelea kudumisha amani. Wamesisitiza kuwa kundi lolote likiona kuna haja ya kudai au kuomba matakwa yoyote, ni wajibu wake kuzingatia kuwa mazungumzo yaendelee na kamwe kwenye vurugu kinachopatikana ni hasara tu.

Wito kwa Serikali:

Taasisi za Kiislamu zimeitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika kuhamasisha vurugu zilizosababisha maumivu na hasara kubwa ya watu na mali, ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Msaada kwa Waathirika:

Pia, wameiomba Serikali kuwasaidia walioathirika na walioumizwa kwa bahati mbaya wakati wa machafuko hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso