*Sekta Madini Kinara Mapato ya Serikali, Kichocheo cha Uchumi, Huduma na Ustawi wa Jamii*
Sekta ya Madini imetajwa Kinara katika kuchangia makusanyo ya Serikali, mapato ya wananchi na uwekezaji kwenye huduma za kijamii kama elimu, afya ikichangiwa na mchango wake kwenye Pato la Taifa kutoka asilimia 6.8 mwaka 2020 kufikia 10.1 mwaka 2024.
*Mambo Mapya*
# Mfuko wa Wakfu wa Madini waja Sekta ya Madini (*Mineral Sovereign Wealth Fund*) Lengo rasilimali madini ilete manufaa kwa vizazi vijavyo kutokana na fedha zitakazotokana na madini badala ya vizazi hivyo kukuta mashimo.
# Madini kudhamini Mikopo ya Uwekezaji ili Madini yatumike kama dhamana.
# Mwaka 2030; Tanzania kuwa kitovu cha mauzo ya Madini yote Afrika Mashariki na Kati. Hii ni kutokana na nchi kubarikiwa aina mbalimbali za madini.
*Mikakati Endelevu*
#Ifikapo mwaka 2030 Kiwanda kikubwa cha Kuchenjua Metali ( Multi purpose Refinery) kuanza. Lengo ni kuongeza thamani madini hapa ..hapa nchini, kuzuia usafirishaji wa makinikia ya madini nje ya nchi na kukoa ajira.
#Serikali kufanya utafiti wa Kina wa madini kutoka asilimia 16 ya sasa ili kuhakikisha Sekta ya Madini inaleta maendeleo na ustawi wa nchi.
#Kongani ya Buzwagi kuzalisha ajira Laki Tatu ( 300,000). Viwanda kupitia Kongani hiyo vitazalisha vipuri na bidhaa mbalimbali lengo ni kuelekea Taifa linalojitemea.
# Serikali kukamilisha Mkakati wa Madini Mkakati utakaosaidia kujua aina ya madini, mahali yalipo, kwa kiasi gani na umakini utawekwa katika kusimamia uwekezaji wa madini hayo kutokana na mahitaji makubwa ya madini hayo duniani.
# Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania ( BoT) kuendeleza utaratibu wa kununua dhahabu kama akiba kutoka kwa wachimbaji wadogo na wa kati wenye Leseni halali lengo ni kuwawezesha kupata masoko, kupunguza utoroshaji wa madini na kurasimisha biashara ya uchimbaji kwa vijana.
#Serikali kukamilisha ujenzi wa jengo la Tanzanite Exchange Center Mirerani.
#Serikali kuimarisha masoko ya Madini na vito.
# Serikali kupitia upya Leseni zisizoendelezwa na kupatiwa wenye dhamira ya kuziendeleza
# Serikali kuendelea kuwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuwapatia maeneo ya kuchimba, mitambo na taarifa sahihi za kijiolojia.
*Madini ni Maisha na Utajiri*
*Madini ni Ajira, Uchumi na Maendeleo*
*Madini Yatatutoa*




No comments:
Post a Comment