UHARIBIFU WA MALI ZA UMMA NI DHAMBI INAYOVUNJA AMRI YA MUNGU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 25 October 2025

UHARIBIFU WA MALI ZA UMMA NI DHAMBI INAYOVUNJA AMRI YA MUNGU




Uharibifu wa Mali za Umma Ni Dhambi Inayovunja Amri ya Mungu


Kiongozi mmoja wa kiroho nchini wametoa wito mzito kwa vijana, akiwataka kuachana na tabia hatarishi ya kuharibu mali za umma au za Serikali kama njia ya kushinikiza mabadiliko.


Amesisitiza kuwa uharibifu wa mali, hata zile za 'mtu mwingine,' si tu kosa la jinai bali pia ni dhambi kubwa kulingana na mafundisho ya Maandiko Matakatifu.


Akizungumza Mchungaji mmoja mashuhuri alisema: "Tunaonya vijana wetu. Kitendo cha kuharibu miundombinu kama barabara, shule, au vituo vya afya, kimefichuliwa wazi wazi katika Biblia kuwa ni kinyume na upendo, haki, na uaminifu tunaotakiwa kuishi nao."


Kanuni za Kibiblia: Kutoka Wizi hadi Uharibifu

Mchungaji alifafanua jinsi Biblia inavyokemea uharibifu na uaminifu katika mambo ya mali,akilirejelea andiko la Luka 16:12, linalosema:"Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?" Alifafanua kuwa:"Mali ya Umma ndiyo mali ya kila Mtanzania, lakini inasimamiwa na Serikali – yaani, 'mali ya mtu mwingine' kwa maana ya msimamizi. Ukiharibu basi wewe ni mdanganyifu na huna uaminifu."


"Uaminifu katika vitu vidogo (au vya 'mtu mwingine') ndio lango la baraka na uaminifu katika mambo makubwa unayohitaji." alisema.


Kukataa Tamaa na Kuepuka Upotevu

Kiongozi huyo wa kiroho aliwaonya vijana dhidi ya kufanya maamuzi yanayoongozwa na 'tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru' zinazoongoza kwenye 'upotevu na uharibifu,' akitumia maneno kutoka 1 Timotheo 6:9-10."Kushinikiza mabadiliko kwa kuharibu mali ya taifa ni 'wazo potofu' linalotokana na tamaa mbaya," alisema.


"Mabadiliko yanapatikana kwa amani, kwa sanduku la kura, na kwa hekima – si kwa laana ya uharibifu. Mali tunazoharibu leo ndizo tunazihitaji kesho!"


Heshima kwa Mamlaka na Sheria


"Kwa kitendo cha kuharibu mali za umma, kijana anavunja Amri ya Nane ('Usishuhudie uongo'), kwa kuwa mara nyingi uharibifu huendeshwa na uongo na ushawishi," alisema.


Alisisitiza kuwa sheria za nchi na utawala uliopo unapaswa kuheshimiwa, kwani Warumi 13:1 inafundisha juu ya kujitiisha kwa Mamlaka.


Onyo la Kiroho: Laana ya Kuenda Kipotofu


"Biblia inatufundisha kuwa dhambi ni uvunjaji wa sheria (1 Yohana 3:4). Kila anayeendelea kufanya dhambi ni mali ya Mwovu. Tusifanye mambo yetu kwa kufuata tamaa mbaya na kuleta uharibifu. Hii inakwenda kipotofu na matokeo yake ni laana kwa maisha ya mtu binafsi na taifa zima."


Alisisitiza kuwa vijana wanapaswa kutumia nguvu na akili zao kujenga na kuunda, si kuharibu, ili kuepuka laana na kuingia katika baraka za Mungu za uaminifu na ustawi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso