RC MBONI AKABIDHI MAGARI MATANO KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 20 October 2025

RC MBONI AKABIDHI MAGARI MATANO KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI SHINYANGA


Na Marco Maduhu,SHINYANGA


MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita,amekabidhi Magari Matano, kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Shinyanga,ambayo yataongeza ufanisi wa utendaji katika kukabiliana na majanga mbalimbali na kuokoa watu na mali zao.


Amekabidhi Magari hayo leo Oktoba 20,2025,katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa huo.
Amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,kwa kuendelea kuyajali Majeshi,na hata kutoa Magari hayo kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Shinyanga ambayo yataongeza chachu ya utendaji kazi.


“Katika Mkoa wa Shinyanga tumepewa Magari Saba,lakini leo nakabidhi Magari Matano ambayo ndiyo yamefika,gari moja nila kuzimia moto,mawili ya kubeba majeruhi,Jingine la kufanya mawasiliano(Control Unit),nala kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kukabiliana na majanga,”amesema Mboni.


Aidha,ametoa wito kwa wananchi, kwamba kwenye shughuli zao za ujenzi na uwekaji wa miundombinu, walishirikishe Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,ili wapate ushauri na kupunguza athari za majanga.
Naye Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Shinyanga Thomas Majuto,amesema Magari hayo yamewaongeza ufanisi mkubwa wa utendaji kazi na hata kufika kwa haraka kwenye majanga na kufanya maokozi.


Amesema awali kwa mkoa mzima wa Shinyanga, walikuwa na Magari Mawili tu ya kuzimia Moto,lakini sasa hivi yamefika Matatu,pamoja na kupata Magari ya kubeba Majeruhi ambayo hawakuwa nayo kabisa.


TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Shinyanga Thomas Majuto akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita (kulia)akikata Utepe kwenye hafla ya kukaibidhi Magari hayo wa Jeshi la Zimamoto, (katikati)Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamdun,(kushoto)Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga Thomas Majuto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akitest mitambo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akipima presha kwenye gari la kubeba Majeruhi ambalo amelikabidhi kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Shinyanga.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso