
Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Fadhil Nkulu, amepokea Mwenge wa Uhuru 2025 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamad Mbega, leo tarehe 06 Oktoba 2025, katika kata ya Itindi, wilayani Songwe.
Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo, Mhe. Nkulu alisema Mwenge wa Uhuru utapita umbali wa kilomita 89 ndani ya Wilaya ya Songwe, ambapo utakagua, utazindua na utaweka mawe ya msingi katika jumla ya miradi 8 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 6.8.
Miradi hiyo ni pamoja na Uzinduzi wa madarasa 6 na ofisi 2 katika Shule ya Sekondari Kanga,Kutembelea mradi wa nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Kanga, Kuweka jiwe la msingi mradi wa maji Kaloleni, Kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kilomita 2 Mkwajuni, Kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Soko la Madini la Wilaya, Kutembelea mradi wa kikundi cha vijana cha usafirishaji mizigo (Maguta), Kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Zahanati ya Kitongoji cha Miembeni, Kuzindua kiwanda cha uchenjuaji wa madini ya dhahabu (Elution Plant).
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2025:
"Shiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu."
No comments:
Post a Comment