DC NKINDA AAGIZA KUREJESHWA KWA MIPAKA YA KIWANJA CHA MARUHE KULINGANA NA HATI YAKE ILIVYO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 9 September 2025

DC NKINDA AAGIZA KUREJESHWA KWA MIPAKA YA KIWANJA CHA MARUHE KULINGANA NA HATI YAKE ILIVYO

 

Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Frank Nkinda, akimuagiza Ofisa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Kahama, Mashili Magesa, kurejesha mpaka wa kiwanja 
cha mwananchi Tenth James Maruhe kama ilivyokuwa awali


Neema Nkumbi - Huheso Digital Kahama


Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Frank Nkinda, amemuagiza Ofisa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Kahama, Mashili Magesa, kurejesha mpaka wa awali wa kiwanja cha mwananchi Tenth James Maruhe baada ya kugundulika kuwa kilipitiwa kimakosa na barabara.

Akizungumza wakati wa kutatua mgogoro huo katika eneo la Busoka, Nkinda amesema mmiliki wa eneo hilo alipoteza haki yake baada ya kiwanja chake kuingizwa kinyume cha sheria kwenye barabara, jambo lililosababisha kupungua kwa mipaka ya viwanja vya Maruhe.

"Barabara ipite baada ya eneo lake ambapo sheria inamtambua kwamba ni eneo lake, haya ni maelekezo na tunahitaji utekelezaji wa haraka, hatutaki kufika mpaka uchaguzi utekelezaji haujafanyika pia wananchi hawa msiwabughudhi kabisa", amesema Nkinda

Awali, Ofisa Ardhi Mteule, Magesa, amekiri kuwa kulikuwa na makosa ya upimaji wa awali na kueleza kuwa baada ya kugundua dosari hizo, mamlaka ilifanya vikao na wananchi ili kueleza hali halisi na marekebisho yaliyopaswa kufanyika.

Kwa upande wake, mmiliki wa eneo hilo, Maruhe, amesema kuwa kwa mujibu wa ramani rasmi ya mamlaka husika, eneo lake halikuwa barabara na kuomba kipande hicho kirejeshwe kwani kumeathiri uwekezaji wake.

Aidha, Nkinda amewataka maofisa ardhi kuzingatia weledi na sheria za ardhi katika utekelezaji wa majukumu yao badala ya kuwa chanzo cha migogoro baina ya wananchi na serikali.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso