UTT AMIS YAFUNGUA RASMI OFISI KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 20 August 2025

UTT AMIS YAFUNGUA RASMI OFISI KAHAMA

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora (kulia) wakikata utepe ishara ya uzinduzi wa Tawi la UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga Agosti 20,2025

Na Neema Nkumbi, Huheso Digital – Kahama

Ofisi za UTT Asset Management and Investor Services (UTT AMIS) zimefunguliwa rasmi leo Agosti 20, 2025 katika Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, hatua inayolenga kusogeza huduma za uwekezaji karibu zaidi na wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa UTT AMIS, Simon Migangala, amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameweka mazingira bora ya uwekezaji nchini, jambo lililoongeza kujiamini kwa wawekezaji.

“Wakati tunaianza safari hii tulikuwa na mtaji wa shilingi bilioni 100, lakini kwa sasa tumekua kwa kiwango kikubwa kutokana na imani ya wananchi na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na serikali ya awamu ya sita,” amesema Mgangala.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustin Kamuzora, amesema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, mpaka sasa wanasimamia rasilimali zenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 3.5 na wawekezaji wanaokaribia 500,000.

Amesema mifuko ya uwekezaji inayoendeshwa na UTT AMIS imekuwa ikitoa wastani wa faida ya asilimia 12 hadi 15 kwa mwaka kulingana na hali ya soko, jambo linaloendelea kuwajengea wananchi imani.

“Kila mmoja wetu anaweza kuwekeza – iwe katika ngazi binafsi, kwa pamoja (jointly), vikundi, wenye biashara ndogondogo, taasisi au kampuni – na kwa kiasi kidogo kuanzia shilingi 5,000, 10,000 na kuendelea, kulingana na masharti ya mfuko husika. Unaweza kuwekeza wakati wowote na popote kupitia simu na benki. Pia, ukihitaji kutoa fedha zako, unaweza kutoa zote au sehemu yake na malipo yakafanyika ndani ya siku tatu hadi kumi za kazi kulingana na mfuko uliowekeza,” amesema Prof. Kamuzora.

Pia, amebainisha kuwa UTT AMIS tayari ina matawi katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma na Zanzibar, na sasa imefungua tawi la Kahama kutokana na jiografia yake ya kibiashara.

“UTT AMIS ni taasisi nzuri inayotajirisha. Tunaamini kituo hiki kitakuwa chachu ya wale wote wenye fedha kuziongeza maradufu. Ukiwekeza unakuwa na uhakika wa utajiri wako, hivyo tunaamini kabisa kituo hiki kitazalisha matajiri. Uzuri ni kwamba hiyo fedha ni yako na ukiihitaji muda wowote tunakupatia,” ameeleza Prof. Kamuzora.

Prof. Kamuzora ameongeza kuwa UTT AMIS inatekeleza malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa vitendo, ikidhamiria kuongeza kipato cha mwananchi na kushiriki katika kufanikisha ajenda mbalimbali za kitaifa.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Mkinda, amesema uwepo wa tawi la UTT AMIS unaleta fursa ya kipekee kwa wananchi wa Kahama na maeneo jirani.

“Nimefahamishwa kuwa kila mmoja wetu anaweza kuwekeza katika ngazi binafsi, vikundi, wenye biashara ndogondogo, taasisi au kampuni kwa kiasi kidogo kuanzia shilingi 5,000. Unaweza kuwekeza wakati wowote na popote kupitia simu na benki. Pia, ukiamua kutoa fedha zako, unaweza kutoa zote au sehemu yake na malipo yakafanyika ndani ya siku tatu hadi kumi za kazi. Kimsingi, mfuko wa uwekezaji wa pamoja wa UTT AMIS ni kwa ajili ya kila mtu. Tunataka nini tena wana Kahama?” amesema Mkinda.

Aidha, ameiomba menejimenti na wafanyakazi wa UTT AMIS kuhakikisha wawekezaji wa Kahama wanapata huduma za kipekee kwa viwango vya kimataifa ili kuongeza imani na ushiriki wa wananchi katika uwekezaji wa pamoja.

Picha na Kadama Malunde
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora (kulia) wakikata utepe ishara ya uzinduzi wa Tawi la UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga Agosti 20,2025
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora (kulia) wakikata utepe ishara ya uzinduzi wa Tawi la UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga Agosti 20,2025
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora (kulia) wakikata utepe ishara ya uzinduzi wa Tawi la UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga Agosti 20,2025
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda akionesha nyaraka baada ya kufungua akaunti wakati wa uzinduzi wa Tawi la UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga

Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS, Simon Migangala, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS, Prof. Faustine Kamuzora (kushoto) wakizungumza jambo ndani ya Kituo cha UTT AMIS - Kahama Mkoani Shinyanga

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso