MWENYEKITI WA INEC AWAASA WAZALISHAJI WA MAUDHUI KUZINGATIA UKWELI KATIKA TAARIFA ZA UCHAGUZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 3 August 2025

MWENYEKITI WA INEC AWAASA WAZALISHAJI WA MAUDHUI KUZINGATIA UKWELI KATIKA TAARIFA ZA UCHAGUZI

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL DAR ES SALAAM 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mheshimiwa Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, amewataka wazalishaji wa maudhui mtandaoni kuhakikisha wanatoa habari sahihi, zilizofanyiwa utafiti na kuhakikiwa, ili kusaidia kufanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na ufanisi.

Akizungumza leo agosti 3, 2025 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kitaifa baina ya INEC na wazalishaji wa maudhui mtandaoni, Jaji Mwambegele amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika mchakato wa uchaguzi, akieleza kuwa mafanikio ya tume katika utekelezaji wa majukumu yake yanategemea kwa kiasi kikubwa ushirikiano kutoka kwa vyombo hivyo.

"Katika nchi yoyote inayotaka kufanikisha jambo la aina yoyote, vyombo vya habari ni msingi wa kwanza, Kila kinachotolewa na tume hakiwezi kufanikiwa iwapo vyombo vya habari havitaamua kwamba jambo hilo lifanikiwe," amesema Jaji Mwambegele.

Aidha, amewaonya waandishi na wazalishaji wa maudhui dhidi ya kusambaza taarifa zenye maudhui ya uzushi, uchochezi, au lugha za matusi, akisema kuwa hilo linaweza kuhatarisha amani ya nchi na kuharibu mchakato mzima wa uchaguzi.

"Vyombo vya habari vina dhima ya kutoa habari sahihi, za kweli na kwa wakati kuhusu mchakato wa uchaguzi, Ndio sauti ya kwanza ya kuonesha upotoshwaji wa aina yoyote unaofanywa kwa bahati mbaya au kwa makusudi kuhusu tume na zoezi la uchaguzi," amesisitiza.

Jaji Mwambegele amesema kuwa tume ipo tayari kushirikiana na vyombo vyote vya habari katika kutoa ufafanuzi wa taarifa yoyote itakayohitajika, ili kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi kuhusu uchaguzi mkuu ujao.

Mkutano huo umewakutanisha Wazalishaji wa maudhui mtandaoni wakiwemo Bloggers, Youtubers na Wachoraji wa Katuni.

"Kauli mbiu ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni 'Kura yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura"

Picha na Kadama Malunde & Emmanuel Mbatilo
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

O

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso