Na Neema Nkumbi, Huheso Digital – Kahama
Mtangazaji wa Huheso FM Radio, ambaye pia ni Mwakilishi wa Vilabu Wilaya ya Kahama na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Michezo Mkoa wa Shinyanga, Paschal Njamba Malulu, leo Agosti 17, 2025, ameunganishwa kwa ndoa takatifu katika Kanisa la EAGT Mhungula, lililopo Kahama mkoani Shinyanga.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wadau wa vyombo vya habari waliojitokeza kushuhudia tukio hilo muhimu katika maisha ya mtangazaji huyo.
Ndoa hiyo imetajwa kuwa kielelezo cha upendo na mshikamano wa kifamilia, ambapo wachungaji na viongozi wa dini waliwataka wanandoa hao kuishi kwa mshikamano, maelewano na kuheshimiana katika maisha ya kiroho.
Wafanyakazi wenzake wa Huheso FM, Huheso Foundation, Arise and Shine, Huheso Digital pamoja na wadau wengine wa habari walitoa pongezi zao, wakimtakia maisha yenye heri na baraka tele katika safari yake mpya ya kifamilia.
No comments:
Post a Comment