BENJAMEN NGAYIWA, MABULA MAGANGILA NA EMANUEL CHEREHANI WAONGOZA KURA ZA MAONI CCM KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 5 August 2025

BENJAMEN NGAYIWA, MABULA MAGANGILA NA EMANUEL CHEREHANI WAONGOZA KURA ZA MAONI CCM KAHAMA

 

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga, ametangaza matokeo ya kura za maoni yaliyofanyika tarehe 4 Agosti 2025 kwa ajili ya kupendekeza majina ya wagombea ubunge wa CCM katika majimbo ya Kahama Mjini, Msalala, na Ushetu.

Na Neema Nkumbi, Huheso Digital Kahama


Kwa mujibu wa Chatwanga, katika Jimbo la Kahama Mjini, jumla ya wajumbe 6,193 walipiga kura, ambapo kura halali zilikuwa 6,113 na zilizoharibika 80. Matokeo ya wagombea ni kama ifuatavyo:

David Kilala – kura 191
James Lembeli – kura 219
Juliana Kajala – kura 256
Fransis Mihayo – kura 821
Jumanne Kishimba – kura 1,144
Sweetbert Nkuba – kura 1,389
Benjamen Ngayiwa – kura 2,093 (aliyeongoza)

Kwa upande wa Jimbo la Msalala, wagombea walikuwa sita. Kura zilizopigwa ni 7,845, zilizoharibika 160, na kura halali zilikuwa 7,685. Matokeo ni kama ifuatavyo:

Ramadhan Shiganza – kura 105
Edson Masondole – kura 152
Simon Lufenga – kura 189
Ezekiel Maige – kura 791
Amros Kwabi – kura 929
Mabula Magangila – kura 5,518 (aliyeongoza)

Katika Jimbo la Ushetu, wagombea walikuwa wanne,Hadi sasa, matokeo yametolewa ya awali kutokana na kata tatu ambazo zina piga kura leo na kwamba aziwezi athiri matokeo ya ubunge kwa ni wapigakura wote hawazidi elfu 2. Haya hapa ni matokeo ya awali:

Valeria Wilson – kura 153
Machibya Mwambilija – kura 171
Musa Shilanga – kura 452
Emanuel Cherehani – kura 5,656 (aliyeongoza)

Katibu huyo wa CCM, Andrew Chatwanga, amesema kuwa hadi muda wa kutangaza matokeo hakuna malalamiko yoyote yaliyoletwa kutoka kwa wagombea, na wote wamepokea matokeo kwa utulivu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso