ALIYEKUWA MWENYEKITI WA MTAA WA IGOMELO AKAMATWA KWA KUDANGANYA MAUZAO YA ARDHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 22 August 2025

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA MTAA WA IGOMELO AKAMATWA KWA KUDANGANYA MAUZAO YA ARDHI



Na Neema Nkumbi, Huheso Digital – Kahama


Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda, ameagiza kukamatwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Igomelo, Laurent Benedicto, kwa tuhuma za udanganyifu katika mauziano ya ardhi.


Agizo hilo limetolewa baada ya mwananchi mmoja, Emmanuel Maduhu, kumlalamikia Bw. Laurent kwamba aliruhusu kiwanja chake alichokinunulia awali kuuzwa tena kwa mtu mwingine, Maduhu amesema alilipa na kumiliki kiwanja hicho kihalali, lakini alishangaa kugundua kimeuzwa mara nyingine bila ridhaa yake.


Laurent Benedicto amejitetea akidai kuwa Maduhu aliuziwa kiwanja na si kiwanja kilikuwa na boma la nyumba hivyo kiwanja chenye boma la nyumba hakikuhusishwa katika mauzo yaliyofanyika


Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama DC Nkinda, amekataa maelezo hayo na kuagiza Laurent pamoja na mjumbe aliyeshuhudia mauziano hayo kukamatwa hadi pale suluhu ya mgogoro huo itakapopatikana.


Aidha, Mhe. Nkinda amesema migogoro mingi ya ardhi inatokana na viongozi wa serikali za mitaa hivyo amewataka kuacha kuchonganisha wananchi.


"Kuna migogoro mingi ya ardhi karibu kila eneo na ukifuatilia vizuri sisi viongozi tunahusika, haiwezekani sisi tuliopewa dhamana ya kumsaidia Mheshimiwa Rais halafu sisi tunakuwa chanzo cha migogoro ambayo tunawafanya wananchi waichukie serikali yao", amesema Nkinda.


Dc Nkinda amesikiliza kero mbalimbali na kuahidi kushughulikia kero hizo zinazohitaji msaada wa haraka.


Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Frank Nkinda, amezidi kuwafikia wananchi kupitia mikutano ya hadhara ambapo mpaka sasa ameshatembelea maeneo ya Majengo, Nyahanga-Shunu, Mhungula, Mwendakulima na Malunga

















No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso