MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM APONGEZA USHIRIKI WA MKOA WA SHINYANGA KATIKA MAONESHO YA SABASABA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 7 July 2025

MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM APONGEZA USHIRIKI WA MKOA WA SHINYANGA KATIKA MAONESHO YA SABASABA



Sabasaba - Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amepongeza juhudi za Serikali ya Mkoa wa Shinyanga katika kushiriki kwa mafanikio Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Akizungumza baada ya kutembelea banda la Mkoa, Mkurugenzi Elihuruma alisema kuwa banda hilo limekuwa moja ya vivutio vikuu kutokana na ubunifu, ubora wa bidhaa na huduma zilizowekwa kwa ustadi wa hali ya juu.



< /div>

Ameeleza kuwa Mkoa wa Shinyanga umeonesha kwa vitendo utekelezaji wa Sera za Serikali kuhusu uchumi wa viwanda kwa kuunganisha Sekta za kilimo, ufugaji, madini na viwanda vidogo, hatua inayochochea maendeleo jumuishi na ya kikanda. Aliongeza kuwa bidhaa nyingi zilizowasilishwa na wajasiriamali zote zina ubora wa kuuzwa ndani na nje ya nchi, jambo linalodhihirisha matokeo chanya ya sera za Serikali za kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji.




Katika ziara hiyo ya kutembelea mabanda ya Mikoa, Mkurugenzi Elihutuma alisisitiza wajibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuwezesha wajasiriamali, hususan kupitia elimu ya ujasiriamali, miundombinu bora, na upatikanaji wa masoko, ili bidhaa za ndani ziweze kushindana katika soko la kikanda na kimataifa.




“Shinyanga imejipambanua kama mfano bora wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III), unaolenga kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,” alisema Elihutuma.




Ndugu Elihuruma aliwahimiza wadau wa maendeleo na Sekta binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwawezesha wazalishaji wa ndani. Pia aliwataka wananchi wa Dar es Salaam na wageni kutoka maeneo mbalimbali kutembelea banda la Shinyanga ili kujifunza, kuwekeza na kushirikiana katika kukuza bidhaa zinazozalishwa na Watanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso