
Na mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mwili wa mwanaume mwenye umri unaokadiriwa (25-30) ambaye hajafahamika jina wala Makazi amekutwa amefariki dunia katika dimbwi la Maji linalotumiwa kwaajili ya shughuli za Bustani katika mtaa wa Malunga wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Malunde 1 blog imezungumza na baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Maria Frank mkazi wa mtaa wa Malunga amesema aliubaini mwili huo alipokwenda kuchota maji katika dimbwi hilo ndipo akatoa taarifa kwa waendesha pikipiki waliokuwa karibu na eneo hilo.
"Nimechota maji awamu ya kwanza sikuona kitu ila niliporudi kwa awamu ya pili ndio nikaona Mguu unaelea kwanye dimbwi hilo ambalo linatumiwa kwaajili ya kumwagilia bustani katika eneo hili ambalo lipo jirani karibu na shule ya Msingi Malunga,"amesema Frank.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa Marehemu umepelekwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama kwaajili ya Uchunguzi wa madaktari.
"Bado hajajulikana jina wala Makazi,ila nitoe rai kwa Wananchi ambapo kuna madimbwi hatarishi ili kuzuia vifo visivyokuwa na tija,kwani eneo hilo lipo karibu na shule ya Msingi Malunga hivyo ni hatari kwa Maisha ya Wanafunzi,"amesema Magomi.
No comments:
Post a Comment