UKOSEFU WA MAWASILIANO YA SIMU WATESA WANANCHI WA KIJIJI CHA KALOLE, MSALALA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 4 September 2024

UKOSEFU WA MAWASILIANO YA SIMU WATESA WANANCHI WA KIJIJI CHA KALOLE, MSALALA




Na Paul Kayanda, Kahama


Wananchi wa Kijiji cha Kalole, kilichopo katika Halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa mawasiliano ya mitandao ya simu, hali inayosababisha adha kubwa katika maisha yao ya kila siku.


wakazi wa kijiji hicho wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta mawasiliano ili waweze kupiga simu au kutuma ujumbe hali inayopelekea kuathiri shughuli za kibiashara zikiwemo huduma za dharura, na hata mawasiliano ya kawaida kati ya familia na marafiki.


Mmoja wa wana kijiji ambaye hakutaka jina lake lijulikane ameeleza jinsi hali kuwa ukosefu wa mawasilianoni kikwazo kikubwa, hasa kwa wachimbaji wa Dhahabu ambao wanahitaji kuwasiliana mara kwa mara na wenzao kwa ajili ya masuala ya Soko la Dhahabu kama limepanda ama limeshika .


"Inakuwa vigumu sana, hasa wakati wa dharura, unapohitaji msaada wa haraka na hakuna mawasiliano," alisema mkazi huyo .


Mwananchi mwingine Rajab Said ameiomba serikali na makampuni ya mawasiliano ya simu, kuchukua hatua za haraka ili kuboresha miundombinu ya mawasiliano katika eneo hilo ili shighuri zao za kimaenendeleo zisikwame.


"Tunategemea mawasiliano ya simu kwa shughuli zetu za kila siku tunaiomba Serikali kutusaidia kwa kushirikiana na makampuni ya simu ili kutatua tatizo hili," amesema Rajab



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso