TAKUKURU - SHINYANGA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI VIONGOZI NANE-AMCOS - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 31 July 2024

TAKUKURU - SHINYANGA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI VIONGOZI NANE-AMCOS




TAKUKURU MKOA WA SHINYANGA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI VIONGOZI NANE WA AMCOS


Na, Mwandishi wetu


Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga imewafikisha Mahakamani viongozi Nane wa vyama vya Msingi AMCOS,kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa.


Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Julai 31,2024 Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bwana Donasian Kessy amesema taasisi hiyo, imebaini kuwepo kwa vyama vya ushirika msingi 13, vyenye madeni yanayosababishwa na badhi ya viongozi kugushi nyaraka na wengine kutoa fedha kwenye akounti za Chama na kisha kuzigawana kupitia akaunti binafsi.


Amesema TAKUKURU imewabaini watuhumiwa hao kufuatia malalamiko ya wanachama wa chama cha Ushirika kahama Cooperative Union KACU,kukosa malipo baada ya kuuza mazao yao.


Bwana Kessy amesema taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga imewafikisha mahakamani viongozi nane wa vyama vya Msingi vya Kangeme na Mshindi kwa makosa hayo ya kujihusisha na vitendo vya rushwa.


Ameeleza kuwa kesi nne zinaendelea mahakamani huku Jamhuri ikishinda katika shauri moja, ambapo watuhumiwa wameamriwa kulipa kiasi cha fedha shilingi Milioni 24, ambazo walizipata kwa njia ya rushwa na kwamba tayari wamerejesha shilingi Milioni 12.


Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga amesema taasisi hiyo inaendelea kushughulikia malalamiko katika vyama vingine 11,vya msingi AMCOS ili kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya viongozi wote waliohusika


Taarifa hiyo ni ya utendaji kazi katika robo ya Mwaka iliyoanzia Mwezi April hadi June 2024.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso