WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAPEWA SEMINA MRADI BOMBA LA MAFUTA “EACOP” - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 8 June 2024

WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAPEWA SEMINA MRADI BOMBA LA MAFUTA “EACOP”


WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAPEWA SEMINA MRADI BOMBA LA MAFUTA “EACOP

Na Marco Maduhu,SHINYANGA


Abbas Abrahamu kutoka EACOP.


WAANDISHI wa Habari Mkoa wa Shinyanga, wamepewa Semina ya Maendeleo ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP),kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga-Tanzania.


Semina hayo yametolewa leo Juni 7,2024 Mjini Shinyanga.
Afisa Mawasiliano ya Nje (External Communication Officer) Abbas Abrahamu kutoka (EACOP), amesema Mradi huo eneo kubwa asilimia 80 lipo nchini Tanzania na 20 Uganda, na Tanzania linapita katika Mikoa Nane ambayo ni Kagera,Geita,Tabora,Singida,Dodoma,Manyara, Shinyanga na Tanga.


“Tunatoa Semina hii kwa Waandishi wa habari juu ya Maendeleo ya Mradi huu wa Bomba la Mafuta (EACOP),ili kuwafahamisha wananchi hatua ambazo zinaendelea na faida za Mradi huu,”amesema Abrahamu.
Cecilia Nzeganije kutoka EACOP.


Amesema kwa wananchi wote ambao wamepitiwa na Mradi huo wa (EACOP) asilimia 99 wameshalipwa fidia, na waliosalia ni wale ambao wana Migogoro ya kifamilia ikiwamo Mirathi.


Aidha, amesema utekelezaji wa Mradi huo hadi sasa umefikia asilimia 29, na wananchi wengi ambao ni wazawa wamepata ajira.
“Serikali ya Tanzania ina Hisa kwenye Mradi huu, hivyo Sisi Watanzania tuuchukulie Mradi huu ni Wetu Sote sababu Kodi zetu ndiyo zinatumika kwenye utekelezaji wake, hivyo tuutunze na uje kutuletea maendeleo makubwa ya kiuchumi,”amesema Abrahamu.


Mratibu Mahusiano kwa Jamii kutoka (EACOP) Cecilia Nzeganije, amesema kwa Mkoa wa Shinyanga wilayani Kahama, kwamba wananchi waliopitiwa na Mradi huo 619, na waliopoteza Makazi yao ni 12, waliokubali kujengewa nyumba watu 10, huku wawili wakitaka walipewa pesa zao ili wakajenge wenyewe, huku wananchi wengine tayari wameshalipwa fidia zao.
Nao baadhi ya Waandishi wa habari, wamesema Semina hiyo imewajengea uwezo na kufahamu utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP), ambayo yatawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao katika Mradi huo wa kimkakati.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Waandishi wa Habari Shinyanga wakiendelea na Semina Mradi wa Bomba la Mafuta EACOP.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Picha ya pamoja zikipigwa.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso