KAGERA YAJIPANGA KUTEKELEZA PROGRAMU JUMUISHI YA TAIFA YA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO NGAZI YA KATA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 27 March 2024

KAGERA YAJIPANGA KUTEKELEZA PROGRAMU JUMUISHI YA TAIFA YA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO NGAZI YA KATA

Mkoa wa Kagera tayari umetekeleza Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) katika halmashauri zote nane za mkoa huo, na imeanza utekelezaji katika ngazi ya kata.
Baadhi ya washiriki katika kikao cha mapitio


NA MUTAYOBA ARBOGAST, HUHESO DIGITAL, BUKOBA


Programu hiyo iliyoanza 2021/22 ikitarajiwa kukamilika 2025/26, inazileta pamoja wizara na sekta zote zinazomhusu mtoto, pamoja na wadau katika kuhakikisha watoto miaka 0 hadi nane wanafikia ukuaji timilifu.


Taarifa ya utekelezaji huo imetolewa na mratibu wa mkoa wa PJT-MMMAM, Issa Mrimi, tarehe 25 Machi 2024, katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba, wakati wa kikao cha mapitio ya utekelezaji wa Progamu hiyo kwa robo ya mwaka,Oktoba-Desemba 2023, kikao kilichowahusisha wataalam ngazi ya halmashaur za wilaya na mkoa,mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa vituo vya kulelea watoto wadogo.


Suzan Mkondya,Afisa ustawi wa jamii kutok wilaya ya Karagwe, ameijulisha kuwa zoezi la kupeleka elimu ya MMMAM iilikwishaanza kwa ngazi ya kata zote 23, baada ya kuwa halmashauri hiyo imefikiwa na kamati ya mkoa, na zoezi hilo ni endelevu.


Shirika la TADEPA la mkoani hapa linalohusika pia na programu hiyo, limeishukuru halmashauri ya wilaya ya Karagwe katika maandalizi waliyofanya kupokea programu kwa kuwashirikisha Baraza la madiwani, jambo lililosaidia elimu hiyo kusambaa, na kuziomba halmashauri nyingine kuwa na mikakati ya kuieneza programu kwa vitendo.

Picha ya pamoja washiriki wa kikao cha mapitio  ya utekelezaji PJT-MMMAM  mkoa wa Kagera


Evance Mvungi, Afisa ustawi wa Jamii toka halmashauri ya Missenyi, amesema kwa robo ya Oktoba Desemba 2023, walimu 60 wa madarasa ya awali walipatiwa mafunzo, na pia watoto 900 chini ya miaka 5 walipatiwa vyeti vya kuzaliwa, na kufikisha watoto 32,000 waliopata vyeti hivyo tangu Julai 2023 kiasi kwamba hakuna mtoto ambaye hakusajiliwa.


Johanitha Jovin, Afisa Lishe wa mkoa wa Kagera amewahimiza wadau kutumia bajeti inayotengwa na serikali kwa halmashauri kutoa umuhimu kwa programu hii, na pia kutumia vikao vya kawaida visivyohitaji bajeti maalum, kutoa kipaumbele juu ya maendeleo ya watoto.


Kikao kimeazimia halmashauri zote kufikia elimu hiyo ngazi ya kata na pia kila halmashauri kufanya mapitio ya utekelezaji kila robo ya mwaka.


Dr Martin Rwabilimbo kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa, akifunga kikao hichò, amehimiza matumizi sahihi ya data na takwimu katika ripoti za mapitio ya utekelezaji, ili kuhakikisha mipango sahihi ya upatikanaji huduma bora kwa watoto.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso