AKAMATWA KWA MAUAJI YA MPENZI WAKE-NJOMBE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 24 August 2023

AKAMATWA KWA MAUAJI YA MPENZI WAKE-NJOMBEJeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Samwel Nduluhundu (38) mkazi wa Mtaa wa Ramadhani Halmashauri ya mji wa Njombe kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Felister Danda (24) ambaye alikutwa ameuawa na kutelekezwa katika misitu ya Tanwat huku mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili akiwa pembeni yake.


Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe, John Imori akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.


Amesema mtuhumiwa huyo alidaiwa kutekeleza mauaji hayo kutokana wivu wa kimapenzi baina ya wawili hao.


Kamanda Imori amesema marehemu na mtuhumiwa huyo walikuwa wapenzi lakini baadae marehemu aliamua kukataa kuendelea na mahusiano hayo jambo ambalo mtuhumiwa hakukubaliana nalo.


"Mtuhumiwa hakukubaliana na maamuzi hayo ya marehemu na kumtaka amrudishie vitu ambavyo aliwahi kumnunulia lakini marehemu alikataa kurudisha akimwambia hata yeye amemtumia,”amesema.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso