ACHOMWA KISU TUMBONI KWA DENI LA TSHS 1,000 SERENGETI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 5 June 2023

ACHOMWA KISU TUMBONI KWA DENI LA TSHS 1,000 SERENGETI


Raphael Juma Matiko (25) mkazi wa Kitongoji cha Kivukoni Kijiji cha Merenga Wilaya ya Serengeti amenusurika kufa baada ya kuchomwa kisu tumboni na utumbo kutoka nje akidaiwa kutomlipa mwenzake sh1000 walizolipwa kwenye kibarua chao.



Tukio hilo limeibua gumzo kubwa kijijini hapo limetokea Juni 4,2023 majira ya saa 1.30 jioni katika Senta ya Nyamieri limethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dk Vincent Mashinji na uongozi wa Kijiji cha Merenga.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Merenga Moses Ryoba akiongea na Serengeti Media Centre na antomatv oline kwa njia ya simu leo jumanne Juni 5 amesema,mtuhumiwa ambaye jina tunalo alikuwa ana mdai majeruhi sh 1,000 baada ya kukutana walizozana akachomoa kisu na kumchoma tumboni hadi utumbo kutoka nje.


“Nilipokea taarifa nikaenda kasi na pikipiki nikamkuta majeruhi utumbo uko nje ikabidi achukuliwe na kukimbizwa hospitali ya wilaya kwa matibabu,wakati huo mtuhumiwa akawa amefungiwa ndani ya nyumba moja kwa usalama,nikamfunga na Kamba kwenye pikipiki yangu na kumpeleka Kituo kidogo cha Polisi Mto Mara kwa hatua zaidi,”amesema.

Akiongea na Kituo hiki majeruhi kupitia simu ya kaka yake akiwa amelazwa hospitali ya wilaya amesema,”Ni kweli jamaa tulipiga naye kibarua nikawa nimechukua hela yake sh1,000 juzi tumeonana nikamwambia ninayo nitampa,lakini jana aliponikuta akaanza kunivuruga akanimwagia bia kichwani,nilipomuuliza sababu akasema anataka buku yake,”amesema na kuongeza,


“Buku nilikuwa nayo mfukoni lakini yeye hakuja vizuri,nami sikutaka kupigana naye maana ni kama kaka yangu maana ananizidi miaka mitatu,ghafla akachomoa kisu na kunichoma tumboni,yaani alitarajia kuniua kwa ajili ya buku”.


Mkuu Wilaya ya Serengeti, Dk.Vincent Mashinji amekemea vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na kudai kuwa ameshaagiza mabaraza ya wazee kushirikiana na polisi kudhibiti vitendo vya uhalifu pamoja na watu kutembea na sime na mapanga.


Polisi Wilayani hapa wamekiri kumshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Chanzo - Serengeti Media Centre

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso