SHIRIKA KINARA,MRADI WA MTOTO KWANZA MKOANI LATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI HABARI MKOANI KAGERA,KUANDIKA KWA WELEDI HABARI ZA WATOTO WADOGO. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 4 March 2023

SHIRIKA KINARA,MRADI WA MTOTO KWANZA MKOANI LATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI HABARI MKOANI KAGERA,KUANDIKA KWA WELEDI HABARI ZA WATOTO WADOGO.

WAANDISHI wa habari watano katika Mkoa wa Kagera,wamepatiwa mafunzo ya siku moja, Machi 03,2023,
kupata mwelekeo na weledi katika kuandika habari za watoto wadogo wenye umri wa miaka 0 hadi nane,ikiwa ni hatua mojawapo ya kutekeleza Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM.

Mkurugenzi wa shirika la TADEPA,James Barongo Bashweka akiwasilisha mada kwa waandishi habari.


Na Mutayoba Arbogast,HUHESO DIGITAL,Bukoba


Mafunzo hayo yametolewa na shirika la TADEPA(Tanzania Development and AIDS Prevention)la mkoani Kagera,linalotekekeza mradi wa Mtoto Kwanza chini ya Shirika la Children in Crossfire Tanzania,kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC)na Shirika la Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN),ambao pia kwa pamoja wanatekeleza Programu hiyo jumuishi ya taifa.


Mkurugenzi wa TADEPA, Dr James Barongo Bashweka amewataka waandishi hao kuandika habari kwa usahihi na weledi,lakini akisisitiza juu ya kutafuta ufumbuzi wa masuala mtambuka yanayoathiri maendeleo ya mtoto.


"Haitoshi kuandika kuwa mtoto fulani kabakwa,bali mwende zaidi kwa uchunguzi kujua ilikuwaje,mazingira ya mtoto,mhusika na hali yake,jamii iliyomzunguka,na nini kifanyike.Uandishi wa habari wenye suluhisho (Solution Journalism) utatusaidia kuliko kuabdika kwa kulalamika tu.


Abimeleck Richard,Afisa mradi wa Mtoto Kwanza katika shirika hilo amewaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuwahimiza watunga sera na serikali kwa ujumla kuwekeza raslimali toshelezi kwa watoto wachanga katika afua za elimu,lishe,afya,ulizi na usalama wa watoto ,na ujifunzaji wa awali.


Agnes Joseph,ambaye ni Afisa utumishi wa TADEPA,pamoja na mambo mengine,alisisitiza juu ya unyonyeshaji maziwa ya mama kwa kipindi cha miaka miwili na miezi sita mfululizo na siyo kurukiarukia vipindi fulani kisha mama akajihesabu amenyonyesha kwa muda wa kipindi hicho cha unyonyeshaji.


Naye mwakilishi kutoka Ofisi ya Ustawi wa Jamii mkoani Kagera Ndugu Kepha Elias amewashauri waandishi wa habari kumtumia Afisa habari wa mkoa wanapohitaji viongozi ngazi ya mkoa katika kupata habari na takwimu mbalimbali.


Baadhi ya watoa mada akiwemo mwandishi wa habari hii wamepitia kozi mbalimbali zinazowahusu watoto,ikiwemo Sayansi ya maendeleo ya mtoto(ECD)kutoka Chuo Kikuu cha Aga Khan


Kwa pamoja washiriki wamekubaliana kuunda mpango mkakati kuhakikisha programu inawafikia wananchi kwa wingi,na wameunda Kamati ya liinda na kuboresha maudhui,na kufanya kazi kama timu,huku Mkurugenzi wa TADEPA akiahidi kuwasaidia waandishi hao kufika maeneo mbalimbali mkoani kwa ufuatiliaji na uchunguzi wa masuala ya watoto kadri mfuko utakavyoruhusu,na kuwa waandishi wengine wataongezwa kwenye timu.


Waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ni Anord Deogratias(Kagera Community Radio FM),Theofilda Felician(Radio Karagwe FM,Anord Kailembo(Kwizera FM),Titus Mwombeki(Kasibante FM), na Mathias Byabato,Meneja wa Kagera Community Radio FM.


Baadhi ya washiriki toka TADEOA na waandishi  wa habari

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso