SUMA JKT MKAMILISHE KWA MUJIBU WA MKATABA HAKUNA NYONGEZA YA MUDA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 2 February 2023

SUMA JKT MKAMILISHE KWA MUJIBU WA MKATABA HAKUNA NYONGEZA YA MUDA



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk Selemani Jafo amempa wiki mbili mkandarasi wa kampuni ya Suma JKT pamoja na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linalosimamia kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa ofisi ya Makamu wa Rais kwa muda waliopewa.


Ofisi ya Makamu wa Rais ilisaini mkataba wa Sh18.8 bilioni na Kampuni ya Suma JKT Oktoba 13, 2021 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi iliyopaswa kukamilika Novemba 09, 2022.


Kwa mujibu wa mpango kazi uliowekwa, kazi ya ujenzi huo kwa ujumla uko nyuma hali inayotokana na kasi ndogo ya ujenzi wa jengo hilo kutoridhisha.


Akiwa ameambatana na viongozi na wataalamu kutoka Ofisi hiyo katika ujenzi unaoendelea eneo la Mtumba jijini Dodoma leo Februari 1, 2023, Waziri Jafo ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo hilo na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso