MTOTO WA MIAKA MIWILI ANUSURIKA KUBAKWA NA KIJANA WA MIAKA 21,SHINYANGA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 9 December 2022

MTOTO WA MIAKA MIWILI ANUSURIKA KUBAKWA NA KIJANA WA MIAKA 21,SHINYANGA.

Mtoto mwenye miaka 2 (jina lake limehifadhiwa) mkazi wa Mjimwema Halmashauri ya Wilaya Kahama anusurika kubakwa na Michael Edward (21),mkazi wa mjimwema baada ya kukutwa akiwa amevua nguo na kumpakata mtoto huyo kwaajili ya kumfanyia ukatili huo.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi


Khalima Khoya, Huheso Digital Kahama

Tukio hilo limetokea Desemba 6 Mwaka huu,katika Kitongoji cha Mjimwema Kijiji cha Gembe Kata ya Kagongwa Halmashauri ya Wilaya Kahama Mkoani Shinyanga.


Akizungumza kwa njia ya Simu mwenyekiti wa kitongoji cha Mjimwema,Mitusela Joseph,amesema siku ya jumanne desemba,6,2022 majira ya saa 12 jioni alipata taarifa ya tukio hilo ambapo alifika eneo husika na kukuta wananchi wakiwa wamemkamata kijana huyo,ambapo alichukua hatua ya kutoa taarifa Polisi kwaajili ya kumkamata mtuhumiwa huyo. 


Kwa upande mama mdogo wa mtoto huyo,Joseline Amon,amesema mtoto alikuwa anacheza pamoja na wenzake lakini baada ya muda wenzake waliondoka ndipo alipobaki peke yake na kupelekea mtuhumiwa huyo kupata upenyo wa kumkamata na kumuingiza bafuni kisha kuvua nguo na kumpakata mtoto kwaajili ya kumbaka.


Aidha Joseline Amon,ameiomba serikali kuwachukulia hatua kali wanaume wanaofanya ukatili kwa watoto wadogo huku akiongeza kuwa wakiwaharibu watoto watakuwa wamekiharibu kizazi na taifa la kesho.
 

"Mtoto alikuwa anacheza na wenzake nje baadaye wenzake waliondoka na kumuacha peke yake,ambapo mtuhumiwa huyo alimkamata na kumuingiza bafuni kisha yeye alivua suruali na kumpakata huku akiwa anamvua gauni ili ambake,ambapo baba yake alifika bafuni hapo na kumkuta akitaka kumfanyia ukatili huo,alimkamata na kumpeleka kwa mwenyekiti,Naiomba serikali itumie njia mbadala kuweza kuwalinda watoto ambao ndilo Taifa la kesho"Amesema Bi,Amon.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi,Amethibitisha kutokupata taarifa za tukuo hilo kulingana na majukumu ya kikazi kuwa mengi ambapo amesema atafuatilia ili kufahamu ukweli wa tukio hilo. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso