MIILI YA WALIOFARIKI AJALI YA NDEGE PRECISION AIR YAAGWA,MVUVI ALIYEOKOA ABIRIA ATUZWA NA PIA APATIWA AJIRA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 7 November 2022

MIILI YA WALIOFARIKI AJALI YA NDEGE PRECISION AIR YAAGWA,MVUVI ALIYEOKOA ABIRIA ATUZWA NA PIA APATIWA AJIRA



WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewaongoza wanachi, viongozi wa serikali, dini na vyama vya siasa kuaga miili ya watu 19 waliofariki jana katika ajali ya ndege, Precision Air iliyoanguka katika ziwa Victoria kutokana na hali ya hewa.


NA MUTAYOBA ARBOGAST-HUHESO DIGITAL-Bukoba


Akiwasilisha salaam za pole na rambirambi oka kwa mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, aliyeko ziarani nchi za nje,amesema Rais amemuagiza kijana aliyejitolea maisha yake kuokoa abiria 24, Jackson Majaliwa (20), akabidhiwe kwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi ili apate kazi jeshini.

Mvuvi Jackson Majaliwa wa miaka 20, alieokoa watu 24 kwenye ndege Bukoba, Kagera.

Kijana huyo pia amezawadiwa zaidi ya sh milioni nne na laki tano kutokana na ushujaa wake.


Waziri mkuu amesema serikali itagharamia mazishi,na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi wa kitaalam ukifanywa kujua chanzo hasa cha tukio hilo.


Aidha waziri mkuu amesema wavuvi wengine waliohusika katika uokoaji watapatiwa msaada kuendesha shughuli zao


Katika tukio hilo watu 19 walifariki akiwemo Rubani mkuu Captain Buruhani Rubaga,aliyekuwa astaafu kazi mwaka kesho,na msaidizi wake(First Officer),Peter Omondi,huku abria 24 wakiokolewa.


Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa ufafanuzi wa mkanganyiko wa taarifa waliyoitoa jana kuwa abiria waliookolewa ni 26, lakini kijana mvuvi Jackson Majaliwa, aliyevunja mlango wa ndege kwa kasia kuwaokoa abiria, naye alizidiwa na maji, pia kuna mfayakazi mmoja wa kiwanja cha ndege, kutokana na simanzi kubwa iliyompata, alizimia, hivyo nao walipofikishwa hospitali walihesabiwa kuwa walikuwa abiria,kumbe sivyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso