MADEREVA WAKIMBIA ZOEZI LA UPIMAJI ULEVI KAMANDA AMESEMA WAMEPIGA MAJI HAO TUTAWASAKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 10 November 2022

MADEREVA WAKIMBIA ZOEZI LA UPIMAJI ULEVI KAMANDA AMESEMA WAMEPIGA MAJI HAO TUTAWASAKA

Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, linawasaka Madereva zaidi ya 10 wanaoendesha magari ya mikoani na nje ya nchi waliokimbia kupimwa ulevi pamoja na macho katika kituo kikuu cha mabasi cha Nyegezi
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza Sunday Ibrahimu

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza Sunday Ibrahimu ametoa kauli hiyo mapema alfajiri baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwapima ulevi na macho madereva zaidi ya ishirini akiwa ameshirikiana na madaktari kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa huo ya Sokou toure na kusema zoezi hilo ni endelevu na kwamba waliokimbia watatafutwa.


"Unaona zoezi hili lipo serious lakini baadhi ya madereva wamekimbia, unapokimbia kimbia inaonekana umepiga maji jana na unashindwa kuja kupimwa lakini hautatoka humu ndani tutaruhusu madereva waliopimwa ulevi waliokimbia hatutakubaliana nao" amesema Sunday


Dkt. Elizabeth Makamba ni Daktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure anaeleza umuhimu wa kuwapima macho madereva, "Tumeamua kufanya zoezi hili ili kuangalia afya ya macho ya madereva sababu tunahisi kwamba mojawapo ya sababu ya ajali ni matatizo ya macho hivyo tupo hapa kwa ajili ya kuwapima macho kama dereva haoni vizuri ni rahisi kupata ajali".


CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso