POLISI SHINYANGA WAKAMATA SILAHA, NA VITU VYA MAGENDO,RPC MAGOMI AWAASA WANANCHI KUFIKA KITUONI ILI KUTAMBUA BIDHAA ZAO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 21 November 2022

POLISI SHINYANGA WAKAMATA SILAHA, NA VITU VYA MAGENDO,RPC MAGOMI AWAASA WANANCHI KUFIKA KITUONI ILI KUTAMBUA BIDHAA ZAO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limekamata Bunduki za Kivita AK47 mbili, za kiraia 27(/gun 9,Riffle 5 pamoja na Gobole 15 zilizokuwa zinatumika kutendea uhalifu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionyesha Silaha na Pikipiki zilizokamatwa kwenye Oparesheni zilizofanywa na Jeshi la Polisi.


NA HALIMA KHOYA, HUHESO Digital SHINYANGA.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu Novemba 21,2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema silaha hizo zimekamatwa kufuatia misako na operesheni zilizofanywa na Jeshi la Polisi katika kipindi cha miezi mitatu (3) kuanzia mwezi Septemba 2022 hadi mwezi Novemba 2022.


Aidha jeshi hilo mbali na kukamata silaha hizo pia limefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya Heroine kidonge kimoja na kete 10kg,bangi 55kg,mirungi 10kg,mitambi miwili ya kutengeneza pombe haramuya gongo,Tv tatj,mitungi ya gesi 5,majiko ya gesi 4,compyuta 3,subwoofer 6,monitor 3,Darubini 3,king'amuzi kimoja,magodoro 3 na bidhaa mbalimbali za madukani.


Pia Jeshi la polisi Mkoani humo linawaasa wananchi wote kutojihusisha na vitendo vya uhalifu kwa namna yeyote ile ambapo watuhumiwa mbalimbali wanashikiliwa na wwngine wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya aina hiyo.


"Nawaomba wananchi wote mfike katika kituo cha polisi kwanzia Novemba 23,2022 hadi Novemba 30,2022 kwaajili ya kutambua bidhaa zenu tulizozikamata"Amesema Magomi.


Baiskeli na pikipiki zilizokamatwa katika oparesheni 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionyesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa katika oparesheni hiyo mkoa wa Shinyanga.



Baadhi ya Silaha aina ya AK47 mbili, za kiraia 27(/gun 9,Riffle 5 pamoja na Gobole 15 zilizokamatwa katika oparesheni hiyo mkoa wa Shinyanga.

Vitu na vifaa mbalimbali vilivyokamatwa katika oparesheni hiyo Mkoa wa shinyanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso